Mashine za max malipo

Mashine za max malipo

ngomicom

Senior Member
Joined
Jul 6, 2012
Posts
123
Reaction score
19
Wapendwa wana JF, natambua kuwa katika mitaa yetu tayari tunazo mashine za max malipo ambazo zinatumika kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kulipia malipo ya dawasco, luku n.k

Ndugu zangu naomba kujua ukweli wa haya:
  • gharama ya kuzipata mashine ni shiling 850,000?
  • mashine hizi zinatoa pia huduma za M-pesa, Tigo pesa, Airtel money na Ezy-pesa?
  • faida ya mashine hizi ni ndogo kuliko kufanya biashara ya moja kwa moja ya VTL za makampuni ya simu?
Mwisho kabisa naomba ushauri wenu, je zinafaa kuendelea kununuliwa kutoa huduma mtaani hasa kwa mtu ambaye hana biashara nyingine, kimsingi atakuwa anaifikiria na kuitegemea hapo hapo.
 
ni kweli inatoa hizo huduma za m-pesa, tigopesa, luku etc, ila ninachojua ni kwamba siyo biashara ya kuleta faida, ni ya kuvutia wateja kama una biashara nyingine, kuna jamaa yangu aliwahi nunua kwa laki tano, but 2yrs ago sasa hivi sijui bei zake

mkuu si kawaone pale Millennium tower...unless wawe wamehama
 
Ni kweli beinakaribia kuwa hiyo. Maana mimi nilinunua kwa 524,000/= na float ya 300,000/=. kwahiyo hiyo ni kama mtaji wako. Si kweli kwamba inafanya huduma zote hizo, kwani M-pesa hakuna, tigo pesa hakuna. ila wanasema kila siku wataanzisha ila naona kama ni story tu. Kuhusu kwamba unaweza kuifanya ni biashara unayoitegemea sidhani kama utaweza. sana uwe na biashara nyingine na hiyo iwe ni moja huduma unazotoa. haiwezi kuwa na faida sawa na ku deal na makampuni ya cm moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom