Mashirika 14 yameitia hasara Serikali kiasi cha Tsh. Bilioni 183.6

Mashirika 14 yameitia hasara Serikali kiasi cha Tsh. Bilioni 183.6

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mashirika 14 ya umma ya kibiashara yamepata hasara katika uendeshaji. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonesha.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Charles Kichere amesema utafiti huo ni katika tathmini ya miaka miwili.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Sh bilioni 22.8 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 31.2. Kampuni ya Mkulazi ilipata hasara ya Sh bilioni 5.8 mwaka 2020/21 na mwaka uliofuata ilipata hasara ya Sh bilioni 14.3.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilipata hasara ya Sh bilioni 26.3 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 11.9.

Kwa mwaka 2020/21, Shirika la Ndege nchini (ATCL) ilipata hasara ya Sh bilioni 36.1 na mwaka 2021/22 Shirika lilipata hasara ya Sh bilioni 35.2.

Zaidi Soma >>>> News Alert: - Rais Samia apokea Ripoti za CAG na TAKUKURU za Mwaka 2021/2022
 
Hivi bosi ya wakurugenzi inakuwa kazi yake ipi??

Miaka miwili mfululizo
 
Shida ya watanzania wakiiba wanaenda kulia mizigo tu wahindi na wajanja wengine wanapiga halafu wanaenda kujenga nchi zao.

Bongo wanakimbilia kuzijenga nchi za wengine na wa ndani wanaishia kupoteza pesa kwenye papa, ndo maana mtaa ule kuna kipindi walikua wanalia moooooooo mtu anakutikisa na pesa ya familia, wewe mchana umepigwa na jua kwa kuzungusha cv jioni unaongezewa presha na gabachori anachezea hisia zako kwenye kubet na plimialigi, halafu hicho ndo utakachoenda kurithisha wanao na wajukuu gabachori anarithisha senti zake
 
Hizo ni hasara au watu wanakula ? Emu tuache kufanyana km WATOTO sema shirika hili watu walikula billion 26, shirika hili watu walikula billion 31, nk sio kusema hasara wakati pesa zinaliwa
Ukisema wamekula sio sawa mkuu, iko hivi.

Je, hasara ya biashara ni nini? Hasara ya biashara hutokea wakati biashara yako ina matumizi zaidi kuliko mapato wakati wa uhasibu. Hasara ina maana kwamba ulitumia zaidi ya kiasi cha mapato ulichopata.

Sasa kwa mf. Shirika la reli inawezekana ukajaza treni mafuta na ukabeba abiria au mzigo kidogo hivyo kupelekea kupata hasara katika hiyo safari husika siku hiyo, n.k

Kwaio inawezekana sehemu ya pesa ya matumizi ikawa imeenda mifukoni kama inavyosema lakini hilo linahitaji uchunguzi wa kina!
 
Kweli walaji ndo wapiga kelele mitandaoni...ripoti imekosa umaarufu kabisaa pamoja na mdudu yote.

Wasingekuwa sehemu ya madudu, na angekuwepo aliyewazibia, kazi ingekuwa moja tu leo...mtandao ungesumbua kwa kufurika makasiriko

Lakini keo kimyaaaaaa;
  • Starz katudhalilisha
  • Taa za uwanja zikamhanithi mtu uwanjani,
  • Ripoti haina jema
  • Bukoba kule haisemwi ukweli
  • Bima ya afya taabuni
  • Ghala za chakula zimefunguliwa, nafaka zazidi kupaa bei
  • Petrol iko karibu na 3,000
  • Uwezo wa milo mi3 umetoweka
  • Mikopo yakufa mtu inaishia kwa walamba asali

Lakini kimyaaaaa kama hamna kitu, ushoga na usagaji washika hatamu, Kamara sio mmoja wao kweli?

Tuendelee tu kumsakama marehemu, pengine tutarudi uchumi wa kati kwa kumtukana yeye.
 
Mashirika 14 ya umma ya kibiashara yamepata hasara katika uendeshaji. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonesha...
Acha watafune tu, ndio wenye nchi hao.
 
Hizo ni hasara au watu wanakula ? Emu tuache kufanyana km WATOTO sema shirika hili watu walikula billion 26, shirika hili watu walikula billion 31, nk sio kusema hasara wakati pesa zinaliwa
Ww ukitengeneza chapati kwa gharama ya 100000 mauzo yakawa 70000 .unanakuwa umekula hiyo 30000??? Chuki na waliosoma we ukiwa unavuta bangi secondary haikufai
 
Ttcl ni haijawahi kua na faida miaka yote kwenye ripoti lazima ifunge na loss
Lakini tulishasema serikali isifanye biashara bali itoe huduma!

Shirika kama la TTCL ni la kutuhudumia wananchi lakini linapogeuzwa la kibiashara ndio shida inakuja! Daima hawawezi kupambana na makampuni binafsi.

Rostam aliuza hisa zake zote za Vodacom baadae kaja kununua hisa za Tigo, unapambanaje na watu wa design hii? Hawa ndo wanacheza na soko na waalijua kindakindaki

Kama serikali inafanya biashara basi Taifa letu linapata hasara kila mwaka kwasababu mishahara tunayowalipa ni tofauti kabisa na wanacho-deliver.
 
Back
Top Bottom