View attachment 927687
Bandari ya Mombasa
Hofu imetanda nchini Kenya kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa, Serikali ya Kenya iko mbioni kuuza Mashirika na Makampuni yapatayo 26 nchini humo kwa Wachina ili kupata fedha za kulipia madeni yanayoielemea Nchi hiyo.
Tume ya Ubinafsishaji imeridhia Mashirika ya Serikali 26 kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali. Miongoni mwao kuna: Benki ya Taifa ya Kenya; Mamlaka ya Bandari ya Kenya; Viwanda vya sukari, nyama na saruji
View attachment 927697
Hivi karibuni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alikuwa nchini China kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara, ambapo China ilitangaza kufungua soko lake kwa ajili ya bidhaa za Kenya. Sasa Wakenya wanahoji, iweje Kenya aruhusiwe pekee huko China, kuna nini Kenyatta alicho-offer kwa Wachina?
Baadhi tayari waneanza kuona ya Zambia yakiingia nchini Kenya, kutokana na mzigo wa madeni hasa kutoka kwa Wachina.
Haya, nyie wanaojidai kuisifia Kenya kwa diplomasia njooni hapa muone faida ya kusafiri kila mara kwenda nje halafu unarudi na mzigo wa madeni.
Kwa haya yanayotokea nchini Kenya, yanathibitisha wazi kuwa, maendeleo huwa hayaletwi kwa sababu Rais ana diplomasia nzuri na anajipendekeza nje. Maendeleo huletwa na usimamizi madhubuti wa mipango mliyojiwekea.
Nafikiria ingekuwa Hali hii ndiyo iko Tanzania, hii taarifa wale waliozaliwa kujua mabaya pekee ya Serikali wangekesha wanashangilia wakidhani anayeumia ni Rais Magufuli na siyo wao. Cha ajabu, kwa hili la Wakenya baadhi ya watu humu nchini wanaumia sana kuiona Kenya katika hali hiyo.
Halafu hawa ndio wanataka waishauri Serikali, never!!!
State to sell 26 companies to finance current budget