Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Na
Victor Wilbard.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia inayohusiana na taarifa a kila mwaka za usafiri wa anga " World Bank Report; Air transport annual report" mwaka 2016 ilionesha kuwa usafiri wa anga unaohusisha hedge za abiria ukiendelea kufanya vizuri katika mataifa yaliyoendelea kwa kufungua milango ya masoko mapya na mahusiano mazuri huku ndege za mizigo zikiendeshwa chini ya matarajio (likiingiza hasara).
Usafiri wa anga uliweza kusaidia kuzalisha ajira zaidi ya milioni sitini na tatu (63 mill) na dola za kimarekani trilioni 2.7 katika GDP ya Dunia. Hali hii huenda ilizifanya Nchi nyingi Duniani ikiwemo Tanzania kuhamasika kuwekeza kwenye usafiri wa anga.
Ripoti hizi zinazotolewa kila mwaka zinaonesha kuwa siyo maeneo yote yanayofaidi ukuaji wa biashara ya usafiri wa Anga mathalani biashara ya usafiri wa anga (Asia -Pacific) ulizalisha faida ya dola za Kimarekani milioni mia tisa US$900 mwaka 2016.
Kwa Afrika usafiri wa anga unaendelea kujiendesha kwa hasara na kushindwa kabisa kujiendesha kwa baadhi ya mashirika kwa mfano mwaka 2016 mashirika ya Afrika yalipata hasara ya dola za Kimarekani milioni mia nane US$ 800
Ripoti hizi zinaonesha hasara katika mashirika ya ndege za Afrika ni jambo linalojirudiarudia katika mashirika mengi.
Kwa Tanzania ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imeendelea kuonesha hasara katika shirika la ATCL .Kwa mfano mwaka wa fedha 2015/16 shirika hili lilipata hasara ya shilingi bilioni 94.3, Mwaka wa fedha 2016/17 hasara iliongezeka na kufikia bilioni 109.3 na Mwaka wa fedha 2017/18 hasara ilikuwa bilioni 113. Taarifa ya mwaka 2020/21 imeonesha hasara ya bilioni 60.
Takwimu hizo za ofisi ya mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali zinaonesha licha ya hasara kuwepo lakini imekuwa ikipungua na taarifa ya mwaka 2020/20 inaonekana kuwa na hasara ndogo kuliko miaka mingine.
Taarifa za kimataifa za usafiri wa anga zinautaja mwaka 2020/21 kama mwaka ambao mashirika mengi ya ndege Duniani yameingia katika hasara kubwa mno na mengine kushindwa kabisa kujiendesha.
Tanbihi: Hasara ni hasara iwe ndogo au kubwa na jambo la muhimu ni kufanya tafiti za kutosha ili kubaini mianya ya hasara na kuipunguza au kuiondoa kabisa ili faida za usafiri wa Anga zidhihirike pia katika Nchi yetu.
World Bank Group (WBG) wanashauri ili kuleta ufanisi katika usafiri wa anga ni vizuri kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya mashirika ya Umma na binafsi katika kujenga miundombinu ya usafiri wa anga.