Mashirika ya haki za binadamu na sheria Afrika Mashariki watoa waraka unaomtaka Rais Samia amuachie Tundu Lissu

Mashirika ya haki za binadamu na sheria Afrika Mashariki watoa waraka unaomtaka Rais Samia amuachie Tundu Lissu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Sakata la Tundu Lissu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa uahini limeendelea kuchukua sura mpya.

Siku ya leo taasisi za haki za binadamu na sheria kutokea Afrika Mashariki yameungana na kutoa waraka wa pamoja wa kukemea na kulaani kukamatwa kwa Tundu Lissu.

Waraka huo ambao umesainiwa na East African Law Society, International Commission of Jurists Kenya, International Commission of Jurists, Law Association of Zambia, Law Society of Kenya, Pan African Lawyers Union, SADC Lawyers Association, Tanganyika Law Society na Uganda Law Society umebainisha mambo tofauti kuhusu kesi hiyo.

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Waraka huo ulisisitiza kwamba kukamatwa kwa Tundu Lissu Lissu chini ya kifungu kinachoruhusu Lissu kuwekwa rumande ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Pia waraka huo umeitaka serikali ya Tanzania, hasa Rais Samia Suluhu Hassan kumuachia Tundu Lissu mara moja ili kurudisha utaratibu wa kidemokrasia na haki uliokuwepo.



ujumbe ngos.jpeg


ujumbe ngos2.jpeg
 
Back
Top Bottom