Bunge wakae chini watunge sheria za kuwajibisha viongozi wa umma maana tunakoelekea ni kubaya sababu kiongozi ukiwa na mapenzi mema na taifa lako kuhakikisha kodi inakusanywa, unapambana na madawa ya kulevya mwisho wa siku wakwepa kodi na walanguzi wa madawa wanawapampu mawakili walianzashe ili viongozi wengine waogope na kwa hatua hii kazi hazitanyika kabisa na kuna watu watakuwa wanakataa teuzi. Mtu kama makonda amepambana sana kwenye kupunguza wimbi la madawa ya kulevya hakuangalia mtu usoni na kwakweli alifanikiwa sana hata kuchochea maendeleo ya Dar es salaam watumishi walikuwa waoga kufanya vitendo viovu kulingana na uongozi imara wa Makonda eti leo anapelekwa mahakamani na ukiangalia washangiliaji wengi ni wale watu wa upande wa pili na wenye elimu za chini(team la saba b) kwamba hawezi kuwa kwenye list za hao viongozi.Ziwepo kamata za maadali au tume ya migogoro kati ya viongozi wa umma na wananchi na iwe na nguvu kisheria mtu asiende mahakamani bila kupitia huko na ikishindikana kesi iende high court.