Mashtaka ya Tundu Lissu ni ya kweli. Tafsiri ya uhaini kwenye katiba ni hii

Mashtaka ya Tundu Lissu ni ya kweli. Tafsiri ya uhaini kwenye katiba ni hii

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
409
Reaction score
343
Wanabodi,

Wanao amini kwamba mashtaka ya Tundu Lissu yanatakiwa yafutwe kwasababu anahukumiwa kwa alicho kisema na sio alicho kifanya wanatakiwa waelewe vifungu vya katiba vinaeleza nini kuhusu uhaini
 

Attachments

  • 2.mp4
    12 MB
Ila kwa hapa tulipofikia kama Taifa, kuja kupata Umoja wa Kitaifa tuna safari ndefu sana.

Bahati mbaya, Wazee wenyewe wa kuliponya Taifa wamebakiza miaka 5 hadi 15 ya kuishi maana wengi umri umewatupa Mkono.

Sina hakika hivi visasi vikihamia Kwa watoto wetu, Nchi itakuwaje

Kwasasa CCM anaona haki akiuawa mtu wa CDM

Itafikia hatua Mtu wa Chadema ataona ni haki yake kutendewa hayo, naye akipata nafasi anaweza kufanya jambo baya Kwa asiye wa CDM

Hizi Siasa zetu, tuone namna sahihi ya kwenda mbele pamoja kabla hawa Wazee wenye Ushawishi hawajalala kimya
 
Wanabodi,

Wanao amini kwamba mashtaka ya Tundu Lissu yanatakiwa yafutwe kwasababu anahukumiwa kwa alicho kisema na sio alicho kifanya wanatakiwa waelewe vifungu vya katiba vinaeleza nini kuhusu uhaini
View attachment 3314345
Mjinga kweli wewe, nikajua una vifungu vya sheriaz wee unaleta watangazaji wa WASAFI?
 
Ila kwa hapa tulipofikia kama Taifa, kuja kupata Umoja wa Kitaifa tuna safari ndefu sana.

Bahati mbaya, Wazee wenyewe wa kuliponya Taifa wamebakiza miaka 5 hadi 15 ya kuishi maana wengi umri umewatupa Mkono.

Sina hakika hivi visasi vikihamia Kwa watoto wetu, Nchi itakuwaje

Kwasasa CCM anaona haki akiuawa mtu wa CDM

Itafikia hatua Mtu wa Chadema ataona ni haki yake kutendewa hayo, naye akipata nafasi anaweza kufanya jambo baya Kwa asiye wa CDM

Hizi Siasa zetu, tuone namna sahihi ya kwenda mbele pamoja kabla hawa Wazee wenye Ushawishi hawajalala kimya
Jambo linaloleta mikwaruzano kati ya vyombo vya usalama na wana CHADEMA ni sheria za nchi kuwa na mianya. Sikatai kwamba polisi wana vielelezo vya kumkamata Tundu Lissu na kumfikisha mahakamani, ila labda sheria inatakiwa kuwa na maelezo zaidi kuhusu kosa hili. Mtu anaweza kukusudia kuleta machafuko nchini na akatekeleza kusudi lake kwa kushawishi watu kumuunga mkono. Mwingine anaweza kufanya kosa hilohilo ila kwasababu ya kukosa umaarufu akashindwa kushawishi umma. Mhaini mwingine anaweza akaamua kwenda hatua nyingine na kuua watu na kusababisha athari kubwa ya mali za watu. Je wahaini wote kwenye mifano niliyotoa wanastahili kunyongwa?. Sheria inatakiwa itoe tafsiri kwa undani zaidi kuhusu makosa yanayoweza kuonekana kuwa uhaini. Adhabu pia zinatakiwa kuwa tofauti kulingana na aina ya uhaini. Yaani: faini, kifungo cha kipindi fulani mpaka kunyongwa kwa uhaini uliokithiri. Mashtaka ya Tundu Lissu yanaendana na kosa la uhaini ila kumnyonga kwasababu ya hotuba za uchochezi alizozitoa ni kitu ambacho kinatakiwa kufikiriwa mara mbilimbili.
 
To me, Zembela is definitely a joke, a big joke in town. 😁
Huwa nikimsikia tuu nacheka sana, nakumbuka enzi zake na marehemu Max, wakikata viuno na enzi za Mango garden, wakiburudisha kabla Twanga Pepeta hawapanda stejini, nikiwashuhudia enzi nikiwa yanki mjini hapo. Kweli watu hutoka mbali. 😁

Kwa iyo sasa hivi ndio mchambuzi wa masuala nyeti ya nchi hii. 😁
 
Mbona watu hamchambui vifungu vya katiba vilivyosomwa, badala yake mnawachambua akina kitenge waliovisoma? Au walikuwa wanasoma machapisho yao tu ya mitandaoni? Hivi nchi hii aliyeturoga ni nani?
 
Back
Top Bottom