Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo

Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo

Simba watapindua Meza, wana 2 za ugenini, mashujaa watakoma wakija mechi ya marudiano.
Kikosi ni kipana.
 
DvWvPeKWsAEmIZe.jpeg
 
Simba watapindua Meza, wana 2 za ugenini, mashujaa watakoma wakija mechi ya marudiano.
Kikosi ni kipana.
Hiyo inaitwa nitolee

Licha ya msemaji wa Simba Haji Manara kutamba kuwa wana kikosi kipana kinachoweza kucheza michezo miwili kwa wakati mmoja, mambo yamewaharibikia tena baada ya Simba kuchapwa mabao 3-2 na Mashujaa Fc ya kutoka mkoani Kigoma katika mchezo wa kombe la FA (ASFC) raundi ya tatu uliopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Simba imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA katika raundi ta tatu, kama ilivyokuwa msimu uliopita walipoondoshwa na Green Worriors.

Sasa Simba italazimika kutwaa taji la ligi kuu ili iweze kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Swali ni kwamba Papaa Mwinyi Zahera anayeongoza ligi dhidi yao kwa tofauti ya alama 17 atakubali hilo jambo litokee? Kuna kila dalili hawatapanda ndege msimu ujao!

Matokeo ya mchezo mwingine uliopigwa leo, Mtibwa Sugar imeilaza Kiluvya United kwa mabao 3-0
 
Hawa vijana wakikaa benchi wanalalamika, wakipewa nafasi ndio hivyo hawajitumi kabisa.
Simba ina mazingira yote ya kuwezesha kucheza mpira, umri wao bado mdogo.
Simba ya sasa haihitaji wachezaji kama hawa tuliowaona leo.
Wapelekwe hata kwa mkopo kwenye timu nyingine.
Ona Chama anaingia na kupiga faulo vizuri inayosababisha goli la pili.
Kichuya anakimbilia kupiga mpira wa faulo huku akijua kabisa mashuti yake yote hayalengi goli, kwanini hamuachii Kwasi.
Ivi huko mazoezini wanafanya nini ?
Mashuti kumi na moja yote yanatoka nje ?
Hawa vijana wameidhalilisha sana timu ya Simba leo. Yaanii pamoja na stahiki zao zote wanafungwa na wanakijiji ambao hata mshahara hawana. Wanacheza kwa kujitolea tu.
Ni aibu Kwao
 
Mkuu nyie mna kikosi kipana mnacheza hata Ligi 2 Zanzibar na bar according to hajji
 
Back
Top Bottom