Masihi alipita hapa: Siri ya lango lililofungwa Yerusalemu

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,678
Reaction score
27,653
Katika historia ya wokovu iliyoandikwa ndani ya Maandiko Matakatifu, mojawapo ya maeneo ya kipekee na ya kushangaza sana ni Lango la Mashariki la Yerusalemu, maarufu pia kama Lango la Dhahabu (The Golden Gate).

Lango hili linahusishwa moja kwa moja na kuingia kwa Masihi katika mji mtakatifu wa Yerusalemu, ikiwa ni sehemu ya utimilifu wa unabii wa zamani kuhusu Mfalme atakayekuja kwa jina la Bwana.

Kupitia makala hii, tutachunguza kwa kina unabii wa nabii Ezekieli, ushuhuda wa Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu, na uthibitisho wa kihistoria wa leo hii kuhusu lango hilo lililofungwa kama alivyotabiri nabii wa Mungu miaka mingi kabla ya tukio hilo.



1. Unabii wa Ezekieli kuhusu Lango la Mashariki

Katika kitabu cha Ezekieli, tunakutana na maneno ya ajabu sana kuhusu lango hili

“Ndipo alinileta tena kwa njia ya lango la nje la patakatifu, linalotazama upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa. Bwana akaniambia, ‘Lango hili litafungwa; halitafunguliwa, wala mtu yeyote hatapita kulipitia; kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, amepita kulipitia; kwa sababu hiyo litafungwa.’”
— Ezekieli 44:1–2

Andiko hili linatangaza wazi kuwa kwa sababu Bwana Mungu wa Israeli (ambaye kwa Wakristo ni Masihi – Yesu Kristo) alipita kupitia lango hilo, basi litafungwa na halitaruhusu mtu yeyote kulipitia tena.(Hilo andiko linathibitisha pia YESU ni Mungu )



2. Yesu Kristo aingia Yerusalemu kupitia Lango hilo

Katika Injili, tunasoma tukio maalum wakati Yesu aliingia Yerusalemu siku chache kabla ya kusulubiwa. Tukio hilo linatambulika ambapo watu walimkaribisha kama Mfalme,Yesu akiwa amepanda mwanapunda

📖 “Siku ya pili, mkutano mkubwa wa watu waliokuja kwenye sikukuu waliposikia kwamba Yesu anaingia Yerusalemu, walichukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumpokea, wakapaza sauti: ‘Hosana! Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!’”
— Yohana 12:12–13(Hii ni miaka zaidi ya 600 baada ya unabii wa EZEKIEL)biblia tamu sana

Katika mila za Wayahudi, siku hiyo ilikuwa ni ya kuchagua wana-kondoo wa Pasaka.

Kwa hiyo, Yesu aliingia Yerusalemu kama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu akipitia Lango la Mashariki, lililokuwa njia ya kuingia kwenye Hekalu kutoka Mlima wa Mizeituni.



3. Uthibitisho wa kihistoria kuhusu Lango la Dhahabu

Leo hii, lango hilo bado lipo na limefungwa kabisa kwa mawe.

🔹 Historia inaonesha kwamba mwaka 1541, Sultani Suleiman kutoka Dola ya Kiosmani (Ottoman Empire) alitoa amri ya kulifunga lango hilo kabisa. Tangu wakati huo hadi sasa, halijawahi kufunguliwa tena.
🔹 Si hayo tu kwa hofu ya kuja kwa Masihi wa Kiyahudi kupitia lango hilo, Waislamu waliweka makaburi mbele yake, wakiamini kwamba Kuhani au Masiha hastahili kupita karibu na wafu, kwa kuwa angetia unajisi.(Hakujua kama anatimiza unabii ulioandikwa na Ezekiel zaidi ya miaka 2000 iliyopita)


Hii yote ni uthibitisho halisi na unaoonekana leo kwamba unabii wa Ezekieli umetimia. Hakika, maandiko hayawezi kuvunjwa.


4. Maneno ya Yesu kuhusu uthibitisho wa Maandiko

Yesu alisema:
📖 “Na Maandiko hayawezi kuvunjwa.”
— Yohana 10:35

Kwa maneno haya, Yesu alisisitiza kwamba kila neno lililoandikwa katika Maandiko Matakatifu, hasa yale yanayomhusu, ni lazima litimie.

Hili linadhihirika wazi katika suala la lango la Mashariki – alilopitia kama Masihi na Mungu wa Israel sawa sawa na maneno ya nabii EZEKIEL lililofungwa baadaye kama ishara ya utukufu wa Mungu uliopita njia hiyo.

Wakati baadhi ya watu wanahoji uhalali wa Biblia wakidai kuwa imechakachuliwa, ni muhimu kufahamu kwamba:

📜 Biblia ina maelfu ya manuscript (maandiko ya kale) kama vile:

Dead Sea Scrolls

Codex Sinaiticus

Codex Vaticanus


Manuscript hizi zingine zimeandikwa hata kabla ya Yesu kuzaliwa, na zingine karne chache baada ya huduma yake duniani.

Kwa mujibu wa ulinganifu wa kitaaluma, maandiko ya leo yana zaidi ya 99% kufanana na maandiko hayo ya kale, jambo linalothibitisha uaminifu wa Biblia kama Neno la Mungu.
 
Quran Haina manuscript,Haina mtiririko wakueleweka ,huwezi kujua historia na matendo ya Musa unayapata wapi,Daudi ,n.k

Huwezi kujua Mungu ana mpango gani na wanadamu
Hapo nimekupata
 
Angalau umekuwa wa faida katika ufalme wa Mungu
Umeachana kwa muda na wale matapeli akina Aterta
 
Biblia ambalo ni neno la Mungu, li hai. Linaishi siku zote, nao waliohaliwa na Roho wa Mungu, wanauona utimilifu wa neno la Mungu kwa kila siku waishiyo.
 
Nje ya Mada.

Wenzetu wamefanikiwa sana kutunza historia yao.

Sisi tunajua pale Isimila Iringa , kuna kumbukumbu za mababu zetu.

Mifupa na zana za jadi ambazo walitumia maelfu ya miaka . Na nadhan hatuvienz ipasavyo.
 
Nje ya Mada.

Wenzetu wamefanikiwa sana kutunza historia yao.

Sisi tunajua pale Isimila Iringa , kuna kumbukumbu za mababu zetu.

Mifupa na zana za jadi ambazo walitumia maelfu ya miaka . Na nadhan hatuvienz ipasavyo.
Tumetunza ,maana hata sio zaman sana hayo matukio yametokea ,

Pia hata huko Israel ,n.k kila siku archeologists wanagundua mengi
 
Biblia ambalo ni neno la Mungu, li hai. Linaishi siku zote, nao waliohaliwa na Roho wa Mungu, wanauona utimilifu wa neno la Mungu kwa kila siku waishiyo.
Ukiwa msomaji wa biblia utagundua Kuna Siri nyingi sana zimefichwa humo ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…