Ditram anatakiwa aendeleze kipaji chake na siyo kujichimbia huko kijijini hata kama aliwekeza.
Kwani kuna ubaya gani akiendelea kucheza soka hata timu ndogo za ligi daraja la kwanza ili pate hela ya kula, huku akiwa hatumii yale mamilion aliyovuna akiwa timu kubwa?
Kuna wachezaji wengi wakongwe bado wanacheza soka ili kusukuma maisha. Siyo kwamba wote hawakuwekeza, ila angalau wanataka waendelee kupata chochote, na siku nguvu zikiisha kabisa, basi wanaendelea kula zile hela walizowekeza.
Maisha ya mpira siyo sawa na kuajiriwa serikalini kwamba utastaafu miaka 60. Maisha ya mpira wa kibongo unacheza hadi miaka 40.
Nilikuwa siamini kama kuna wachezaji wakongwe bado wanacheza mpira, mfano Dani Mrwanda, Haruna Moshi Bobani, Mwantika (DTB), Mrisho Ngasa (Ken Gold).
Pia Tshishimbi amecheza ligi daraja la kwanza msimu huu na Tabora United!
Ditram arudi kucheza soka, Ulaya ndio wanastaafu miaka 30 kwa sababu wanakuwa wamevuna pesa nyingi ambazo wanakula mpaka kufa!
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app