Masikini gari yangu niliyoagiza, uchakavu kodi mpya!

Masikini gari yangu niliyoagiza, uchakavu kodi mpya!

heshima kwenu wadau.

nimeumia sana baada ya kusikia bajeti mpya ya serikali.

nimejibana sana na kuagiza ki gari changu.

kupunguza gharama nikatafuta isiyozidi miaka 10 na ya bei nayomudu ili kuikwepa kodi ya uchakavu na.kupunguza gharama.

gari inatarajiwa kufika next month july 14.

serikali imepitisha bajeti mpya ambayo kodi ya uchakavu ni no more 10 years bali.ni 8 years..

hapo haraka haraka kama milion na uchafu imeshaongezeka kwenye kodi niliyopanga.

hii ni zaidi ya kurudishana nyuma.


sijui ushuru mpya utaanzwa kutozwa july 1 st au watasubiri subiri
mwambie aliyekuuzia gari azi-scan hizo documents halafu akupelekee kwa email. ukizipata mpe clearing agent azifanyie taratibu zote kabla ya july 1.
 
Hapana sijawabagua.

Unajuwa mipango ya kwetu hapa iko kinyume nyume. Ikiwa mtu anaweza kulimbikiza mwaka au miaka miwili akanunuwa gari chakavu, basi huyo huyo anaweza kulimbikiza miaka 10 akanunuwa gari mpya.

Ni wakati muafaka sasa, tukaja na financing companies au bank inayojali wenye kipato kidogo. Unaenda wakala unanunuwa gari mpya unakatwa kidogokidogo kwenye mshahara, mradi iwe na comprehensive, na dhamana ni hiyo hiyo gari. Na makato yako yawe sawa na "depreciation" ya gari. Kila mmoja ataibuka mshindi. Gari likifika miaka 12 au 15 ni lazima liwe scrap au vintage.

Ni mipango tu na wenzetu ndivyo wafanyavyo na sasa wamepata soko la scrap zao (magari ya mitumba) kutuuzia sisi kwa bei poa.

Tukifanya hivyo utaona baada ya muda si mrefu tunafunguwa viwanda vya magari japo kuanzia kwa kuunganisha, bila hivyo hatuendelei ng'oo. Tuwe na mtazamo mpana zaidi ya hapa tulipo.

Chuma tunacho, ni wakati muafaka kianze kutumika kuunda magari badala ya kuagiza mitumba kutoka nje kuwanufaisha wengine.

Nasema ningekuwa mimi, mwisho kuagiza gari chakavu ni miaka mitano. Sasa amuwa, unagiza nje au unanunuwa jipya lililoundwa Tanzania. Ni mipangilio ya kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuanza kujitegemea na sio kutegemea.

Tusiwe na ujamaa wa kijinga kama wa Nyerere, kufunga kiwanda cha kuunda matrekta akafunguwa kiwanda cha majembe ya mkono.

Sasa sisi tuuze chuma nje, wenzetu wakatengenezee magari na sisi tuendelee kununuwa mitumba yao? Fikiri!

huyu dada humu JF huwa naona ni mmoja wa wanaochukiwa zaidi. Tofauti yake na wengine wanaochukiwa humu (kama yule jamaa aliyefanya mazoezi gym akapungua akili badala ya kupungua mwili, mwenye umri sawa na mama anna lakini inabidi umuamkie shkamoo) Faiza anachukiwa kwasababu yupo vizuri kichwani the same applies to zitto. Kudos dada upo safi kichwani keep it up me ni mmoja wa wafuatiliaji wakubwa wa michango yako humu jamvini. Je umeshaolewa?
 
daah pole sana mkuu.
Ila kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kuagiza gari nje. Tafadhali tuwasiliane. Iwe ngo au private. Its better ukakutana na mtu akakupa maelekezo mazuri na namna ya kuingiza gari na shipping line gani
uzitumie.

Ushauri mzur
 
Back
Top Bottom