Hapana sijawabagua.
Unajuwa mipango ya kwetu hapa iko kinyume nyume. Ikiwa mtu anaweza kulimbikiza mwaka au miaka miwili akanunuwa gari chakavu, basi huyo huyo anaweza kulimbikiza miaka 10 akanunuwa gari mpya.
Ni wakati muafaka sasa, tukaja na financing companies au bank inayojali wenye kipato kidogo. Unaenda wakala unanunuwa gari mpya unakatwa kidogokidogo kwenye mshahara, mradi iwe na comprehensive, na dhamana ni hiyo hiyo gari. Na makato yako yawe sawa na "depreciation" ya gari. Kila mmoja ataibuka mshindi. Gari likifika miaka 12 au 15 ni lazima liwe scrap au vintage.
Ni mipango tu na wenzetu ndivyo wafanyavyo na sasa wamepata soko la scrap zao (magari ya mitumba) kutuuzia sisi kwa bei poa.
Tukifanya hivyo utaona baada ya muda si mrefu tunafunguwa viwanda vya magari japo kuanzia kwa kuunganisha, bila hivyo hatuendelei ng'oo. Tuwe na mtazamo mpana zaidi ya hapa tulipo.
Chuma tunacho, ni wakati muafaka kianze kutumika kuunda magari badala ya kuagiza mitumba kutoka nje kuwanufaisha wengine.
Nasema ningekuwa mimi, mwisho kuagiza gari chakavu ni miaka mitano. Sasa amuwa, unagiza nje au unanunuwa jipya lililoundwa Tanzania. Ni mipangilio ya kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuanza kujitegemea na sio kutegemea.
Tusiwe na ujamaa wa kijinga kama wa Nyerere, kufunga kiwanda cha kuunda matrekta akafunguwa kiwanda cha majembe ya mkono.
Sasa sisi tuuze chuma nje, wenzetu wakatengenezee magari na sisi tuendelee kununuwa mitumba yao? Fikiri!