Mimi sitaki kuwalaumu moja kwa moja maana najuwa haikuwa hiyari yao ila makampuni yote ya simu ni lazima wawafidie wateja wao na sio kuwafidia na bando sijui wako watu wamepoteza baadhi ya biashara zao au hasara kwa usumbufu huu na mbaya zaidi sio kwamba tatizo la kiufundi hapana wamekata halafu bila kutoa hata notice au kuomba msamaha kama wateja sio lolote lakini wao wateja ndio wanawafanya kuwa wao. Sasa naelewa hapa ni Tz hakitalipwa kitu wala mahakamana zetu hawawezi kutoa adhabu kwa hizi kampuni na mbaya sijui kitengo kinachosimamia haki za wateja. Hawa wangekuwa nchi za wenzetu wangepata habari zao.