Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

kila Jambo na wakati wake, tena ulopangwa na kuthibitishwa na Mungu .

Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake kwa waja wake. Ikiwa amekupangia kupata mtoto ukiwa u18 utapata tu, na vilevile ikiwa amekupangia upate mtoto ukiwa above 60 uta pata tu...

Yote haya ni kwa Neema na Baraka za Mungu tu.
 
Achana nao kenge hao....yaan inashangaza sana “wewe umepata tuliza komwe bas,ya nini kuangaika na sauté nacho” Hizi mambo za kushupalia maisha za watu mtakuja kukutana na mnachokitaka
Kuna watu ni makatili Sana....sio makatili kwa kutumia upanga bali kwa kutumia ndimi zao......wanaongea maneno yanayoishi kwenye vifua vya wenzao kwa uchungu mkubwa Sana.....
 
Hakika ndugu yangu.......

Watu tunajisahau sana......maisha na uzima vinatupa viburi vya ajabu Sana.....mpaka kuwanenea wengine mabaya.......

Mungu atufanyie wepesi na awajaze mioyo ya subira wote ambao hawakujaaliwa kupata neema hiyo.....
 
Kwani Lazima kuoa...
 
Kwani Lazima kuoa...
Ulazima au sio lazima inategemea na utashi wa mtu mwenyewe......na ndio maana ni vizuri kuheshimu maamuzi ya watu kwani hatujui kuna msukumo gani nyuma ya maamuzi hayo.......aliyeamua kuoa au kuolewa inapaswa ayaheshimu maamuzi ya aliyeamua kutokuoa au kuolewa....na sio kusimangana.....
 
Hiyo haiusu mtu ni maisha yake na garama ya anacho atalipia mwenyewe kwann umseme au umkejel
 
Sema sisi Waafrika tuna mambo ya kifala sana.
Mtu ukichelewa kuoa utashangaa watu wanaanza kukushupalia ooh kwanini huoi, unasubiri nini, uzee unakuja nk

Haya, unaamua kuoa.

Mwaka mmoja bila mtoto watu wanaanza ooh mbona hamzai, mna matatizo gani, sijui nini...

Haya, mnapata mtoto

Mwaka mmoja wanaanza ooh, mbona katoto kamoja, ongezeni bana, mnasubiri nini...

Haya, mnapata wapili

Bado tu hawawaachi utasikia ooh mbona watoto wote wa kike, pambaneni mpate na wakiume..!!
 
Yaani ni balaa......
 
Kwa hiyo Mungu ndio hupanga watu kutopata watoto, Na watu wengine kupata watoto?

Huyo Mungu ana upendeleo sana.



Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Religious people especially Christians are worst,hawa viazi wana masimango na judgemental sana kwa ambao bado kuoelwa

Wengine ni newly weds,hawa watu wana masimango sana....majinga kabisa haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…