Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Ukishaanza na hizi habari za Mungu Mungu ukaambiwa Mungu kaamrisha zaeni muongezeke mkaijaze dunia na wewe huna mtoto, tafsiri yake ni mambo mawili tu.

1. Una uwezo wa kuzaa/kuzalisha na hujazaa,/ hujazalisha, umekaidi agizo la Mungu.

2. Huna uwezo wa kuzaa/kuzalisha, na hilo ni matokeo ya laana ya Mungu kwa namna moja au nyingine.

Drop the God talk.

Hiyo habari ya Mungu ndiyo mwanzo wa kunyanyapaa watu wasio na watoto.

Kwenye Abrahamic religions huwezi kutenganisha Mungu na uzazi.
 
Lazima washangae zamani watu walizaa wakiwa na 17 yrs wakichelewa sana 20...siku hz ni kutoa tuu mimba..kaka hataki kuoa na binti hataki mtoto anajiona bado yupo yupo kwanza..wanashauriana watoe..inafika miaka 30 mtoto anatafutwa sasa hapatikani...kaka nae umri umeenda anataka aoe maana kashamaliza ujana ana 50yrs...anazaa uzeeni..
 
Nakubaliana na wewe ndugu.....

Lakini nguzo ya Imani pia tunaamini tumeumbwa kwa kutofautiana maumbile na mambo mbali mbali kwenye miili yetu....katika tofauti hiyo ya maumbile kuna wagumba hawana uwezo wa kuzaa wala kutungisha mimba......

Yote ni maumbile na tunapaswa kumshukuru Mungu kwa maumbile hayo.... lakini pia tunatofautiana utashi wa kuamua mambo kwa jinsi unavyoona au kwa nyakati unazoona zinafaa......ndio maana anaweza kuona kuzaa ni bora akifika 50 kutokana na sababu za kwake yeye mwenyewe na mwingine akaona 25 sio mbaya.....

Wote wako sahihi.....na kuna wengine wanakumbana na adha mbali mbali maishani na kushindwa kufanya mambo kwa wakati....

Hata kwenye dini Mungu hajatuambia umri wa kuoa au kuolewa bali amesema kwa mwenye kuweza kumudu gharama za ndoa na aoe......

Wengine humudu gharama mapema na wengine baadae na hatimaye wote wanatimiza lengo la kuoa na ikiwezekana kupata watoto.......

Kwa hiyo kwa wenye kuamini hivi vitabu vya dini huwezi kuwanyanyapaa wasio kuwa na watoto au wasiooa......
 
Religious people especially Christians are worst,hawa viazi wana masimango na judgemental sana kwa ambao bado kuoelwa

Wengine ni newly weds,hawa watu wana masimango sana....majinga kabisa haya
Ni watu wanaoyatazama mambo kwa utashi wao huku wakijinasibu kama wacha Mungu........

Kwenye ukurasa wa ucha Mungu huwezi kusimanga wala kunyanyapaa mtu kwa vile alivyo......
 
Vigezo ni viwili tu
1. Upo tayari kuingia kwenye ndoa
If YES, ingia

2 Upo tayari kuwa na watoto
If YES, zaa

Kinyume na hapo usifanye hivyo vitu.
Na usisikilize watu wanaongea nini
Hakika ndugu na huo ndio usahihi.......na kila mmoja humkuta ndio kwa wakati wake.....na ndio maana kila mtu hupata ndoa au family kwa nyakati zake.....
 
Wanaume msiotaka kuoa sisi tutawaoa muwe nyumba ndogo. Maana ndio mnachotaka
Pengine mitazamo wako umeakisi mazingira na utashi wako kwa wakati wako.....na uko sahihi kwa ukuta wa fikra zako.......ukitoka nje ya ukuta huo utajifunza mengi na utapanua fikra zako.......

Mungu akufanyie wepesi ndugu
 
Lakin hawa si ndio kataa ndoa hawa?
Wakati mwingine unaweza kuwa na msimamo wa jambo kulingana na ukuta wa fikra zako kwa wakati huo.....ukivuka ukuta huo unakutana mitazamo mipya inayokufunza na kubadili fikra zako na kuwa mtu mpya.......ndio maana wapo waliokula kiapo cha upadri lakini nyakati zilipofika walipigania kutoka kwenye Maisha ya useja.....ni suala la muda Tu.....
 
Hili usemalo hakika ni kwel na nakubaliana na wewe
 
Nguzo ya imani hizo ni contradiction.

So, that does not surprise me.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…