Ivan Stepanov
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 6,799
- 22,209
Lakin hawa si ndio kataa ndoa hawa?kuolewa na kuzaa ni Neema na baraka za Mungu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakin hawa si ndio kataa ndoa hawa?kuolewa na kuzaa ni Neema na baraka za Mungu
Ukishaanza na hizi habari za Mungu Mungu ukaambiwa Mungu kaamrisha zaeni muongezeke mkaijaze dunia na wewe huna mtoto, tafsiri yake ni mambo mawili tu.Habari za muda huu marafiki,
Siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya kushangaza kustaajabisha kwenye jamii yetu na hasa huku mitandaoni.
Kumekuwa na wimbi la watu kuwasimanga, kuwakejeli na hata kuwacheka ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wanaoonekana kwa vigezo, mitazamo na viwango vilivyowekwa kwenye jamii kuwa wamechelewa kuoa au kuolewa hivyo kuonekana wamepata watoto wa uzeeni.
Ni jambo linaloonekana kama la kawaida lakini kwa upande mwingine linasononesha na kuvunja mioyo ya watu walioamua kujenga familia.
Ni kauli za kitoto zinazoonyesha kuwa bado hawajakomaa kiakili kwenye ulimwengu huu uliojaa harakati na purukushani za kila aina.
Ningependa kuchukua nafasi hii kuwakumbusha hao wenye kuwakejeli wengine kwenye hili ya kuwa.
1) Maisha ni fumbo zito Sana ambalo mara nyingi ni wachache Sana wenye kufumbua. Mara nyingi mipango yako inaweza ikapishana na mipango ya Mungu.
2) Uhai na kifo ni vyake Mungu mwenyewe kwani hakuna ajuaye kuwa amebakisha muda gani wa kuishi hapa duniani. Wapo vijana wengi wametangulia mbele za haki wakiacha watoto wao na familia zao zikiteseka na kuwaacha wazee wakiendelea kulea watoto wao wa uzeeni mpaka wakijitegemea na kufurahia matunda yao. Hivyo kusema kuwa mwanaao akifika miaka kadhaa wewe utakuwa umeshachoka au umeshakufa ni maneno ya kufuru au ya mtu asiye na Imani kwa mola wake mlezi.
3) Kwenye maisha kila mtu Mungu amemuwekea wakati wake wa kufanya jambo lake kwa rehema zake. Wapo watu waliowahi kuoa lakini Mungu akawanyima watoto mpaka wanazeeka na wengine wanawapata uzeeni kabisa. Wapo watu wamejikuta wapo jela wakitumikia vifungo virefu na mpaka wanatoka umri umekwenda na wanaamua kujenga familia. Wapo watu walikuwa wanaugua kwa muda mrefu na hatimaye wakapona na kuanzisha familia. Hivyo basi kama wewe umewahi ni sahihi kwako lakini haiwezi kuwa makosa kwa anayeonekana amechelewa.
4) Changamoto za kifamilia na vifo.
Kuna mwingine anawahi kuoa lakini Kati Kati ya safari anawapoteza mke na watoto wote kwa pamoja Kwa ajali au maladhi ya kawaida na anaamua kuoa na kuanzisha familia upyaaa.
Kwa kifupi mambo na changamoto za kidunia ni nyingi zinazopelekea watu kuonekana wamechelewa kupata watoto au kuoa na kuolewa. Tujifunze kuwa wastaarabu kwenye maisha ya watu kwani hatujui matamshi yetu yanawaathiri vipi wenzetu.
Niko tayari kusahihishwa.
Nawasilisha.
kataa ndroa ina muda na umri mkuu...Lakin hawa si ndio kataa ndoa hawa?
Allah angekuwepo, asingehitaji kukumbushwa.
Kila mmoja na anachoamini yeye!Allah angekuwepo, asingehitaji kukumbushwa.
Ukishaona haja ya kumkumbusha tu, ujue hayupo.
Mi naanza kukuoa weweWanaume msiotaka kuoa sisi tutawaoa muwe nyumba ndogo. Maana ndio mnachotaka
Nakubaliana na wewe ndugu.....Ukishaanza na hizi habari za Mungu Mungu ukaambiwa Mungu kaamrisha zaeni muongezeke mkaijaze dunia na wewe huna mtoto, tafsiri yake ni mambo mawili tu.
1. Una uwezo wa kuzaa/kuzalisha na hujazaa,/ hujazalisha, umekaidi agizo la Mungu.
2. Huna uwezo wa kuzaa/kuzalisha, na hilo ni matokeo ya laana ya Mungu kwa namna moja au nyingine.
Drop the God talk.
Hiyo habari ya Mungu ndiyo mwanzo wa kunyanyapaa watu wasio na watoto.
Kwenye Abrahamic religions huwezi kutenganisha Mungu na uzazi.
Ni watu wanaoyatazama mambo kwa utashi wao huku wakijinasibu kama wacha Mungu........Religious people especially Christians are worst,hawa viazi wana masimango na judgemental sana kwa ambao bado kuoelwa
Wengine ni newly weds,hawa watu wana masimango sana....majinga kabisa haya
Hakika ndugu na huo ndio usahihi.......na kila mmoja humkuta ndio kwa wakati wake.....na ndio maana kila mtu hupata ndoa au family kwa nyakati zake.....Vigezo ni viwili tu
1. Upo tayari kuingia kwenye ndoa
If YES, ingia
2 Upo tayari kuwa na watoto
If YES, zaa
Kinyume na hapo usifanye hivyo vitu.
Na usisikilize watu wanaongea nini
Pengine mitazamo wako umeakisi mazingira na utashi wako kwa wakati wako.....na uko sahihi kwa ukuta wa fikra zako.......ukitoka nje ya ukuta huo utajifunza mengi na utapanua fikra zako.......Wanaume msiotaka kuoa sisi tutawaoa muwe nyumba ndogo. Maana ndio mnachotaka
Wakati mwingine unaweza kuwa na msimamo wa jambo kulingana na ukuta wa fikra zako kwa wakati huo.....ukivuka ukuta huo unakutana mitazamo mipya inayokufunza na kubadili fikra zako na kuwa mtu mpya.......ndio maana wapo waliokula kiapo cha upadri lakini nyakati zilipofika walipigania kutoka kwenye Maisha ya useja.....ni suala la muda Tu.....Lakin hawa si ndio kataa ndoa hawa?
Sijui kwa nini baadhi ya watu wana ujinga mwingi sana, kwa nini uumie na uchaguzi wa maisha ya mtu mwingine?Nilicho gundua jamii inataka vijana waoe ili ipate wa kulia wote kuhusu wanawake
Hili usemalo hakika ni kwel na nakubaliana na weweWakati mwingine unaweza kuwa na msimamo wa jambo kulingana na ukuta wa fikra zako kwa wakati huo.....ukivuka ukuta huo unakutana mitazamo mipya inayokufunza na kubadili fikra zako na kuwa mtu mpya.......ndio maana wapo waliokula kiapo cha upadri lakini nyakati zilipofika walipigania kutoka kwenye Maisha ya useja.....ni suala la muda Tu.....
Nguzo ya imani hizo ni contradiction.Nakubaliana na wewe ndugu.....
Lakini nguzo ya Imani pia tunaamini tumeumbwa kwa kutofautiana maumbile na mambo mbali mbali kwenye miili yetu....katika tofauti hiyo ya maumbile kuna wagumba hawana uwezo wa kuzaa wala kutungisha mimba......
Yote ni maumbile na tunapaswa kumshukuru Mungu kwa maumbile hayo.... lakini pia tunatofautiana utashi wa kuamua mambo kwa jinsi unavyoona au kwa nyakati unazoona zinafaa......ndio maana anaweza kuona kuzaa ni bora akifika 50 kutokana na sababu za kwake yeye mwenyewe na mwingine akaona 25 sio mbaya.....
Wote wako sahihi.....na kuna wengine wanakumbana na adha mbali mbali maishani na kushindwa kufanya mambo kwa wakati....
Hata kwenye dini Mungu hajatuambia umri wa kuoa au kuolewa bali amesema kwa mwenye kuweza kumudu gharama za ndoa na aoe......
Wengine humudu gharama mapema na wengine baadae na hatimaye wote wanatimiza lengo la kuoa na ikiwezekana kupata watoto.......
Kwa hiyo kwa wenye kuamini hivi vitabu vya dini huwezi kuwanyanyapaa wasio kuwa na watoto au wasiooa......
Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote, uongo, ukweli, ni haki yako ya kikatiba na kiutu.Kila mmoja na anachoamini yeye!
Yupo na ni mwema sikuzote