Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Habari za muda huu marafiki,

Siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya kushangaza kustaajabisha kwenye jamii yetu na hasa huku mitandaoni.

Kumekuwa na wimbi la watu kuwasimanga, kuwakejeli na hata kuwacheka ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wanaoonekana kwa vigezo, mitazamo na viwango vilivyowekwa kwenye jamii kuwa wamechelewa kuoa au kuolewa hivyo kuonekana wamepata watoto wa uzeeni.

Ni jambo linaloonekana kama la kawaida lakini kwa upande mwingine linasononesha na kuvunja mioyo ya watu walioamua kujenga familia.

Ni kauli za kitoto zinazoonyesha kuwa bado hawajakomaa kiakili kwenye ulimwengu huu uliojaa harakati na purukushani za kila aina.

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwakumbusha hao wenye kuwakejeli wengine kwenye hili ya kuwa.

1) Maisha ni fumbo zito Sana ambalo mara nyingi ni wachache Sana wenye kufumbua. Mara nyingi mipango yako inaweza ikapishana na mipango ya Mungu.

2) Uhai na kifo ni vyake Mungu mwenyewe kwani hakuna ajuaye kuwa amebakisha muda gani wa kuishi hapa duniani. Wapo vijana wengi wametangulia mbele za haki wakiacha watoto wao na familia zao zikiteseka na kuwaacha wazee wakiendelea kulea watoto wao wa uzeeni mpaka wakijitegemea na kufurahia matunda yao. Hivyo kusema kuwa mwanaao akifika miaka kadhaa wewe utakuwa umeshachoka au umeshakufa ni maneno ya kufuru au ya mtu asiye na Imani kwa mola wake mlezi.

3) Kwenye maisha kila mtu Mungu amemuwekea wakati wake wa kufanya jambo lake kwa rehema zake. Wapo watu waliowahi kuoa lakini Mungu akawanyima watoto mpaka wanazeeka na wengine wanawapata uzeeni kabisa. Wapo watu wamejikuta wapo jela wakitumikia vifungo virefu na mpaka wanatoka umri umekwenda na wanaamua kujenga familia. Wapo watu walikuwa wanaugua kwa muda mrefu na hatimaye wakapona na kuanzisha familia. Hivyo basi kama wewe umewahi ni sahihi kwako lakini haiwezi kuwa makosa kwa anayeonekana amechelewa.

4) Changamoto za kifamilia na vifo.
Kuna mwingine anawahi kuoa lakini Kati Kati ya safari anawapoteza mke na watoto wote kwa pamoja Kwa ajali au maladhi ya kawaida na anaamua kuoa na kuanzisha familia upyaaa.

Kwa kifupi mambo na changamoto za kidunia ni nyingi zinazopelekea watu kuonekana wamechelewa kupata watoto au kuoa na kuolewa. Tujifunze kuwa wastaarabu kwenye maisha ya watu kwani hatujui matamshi yetu yanawaathiri vipi wenzetu.

Niko tayari kusahihishwa.

Nawasilisha.
Point sana

Kuna watu wanatamani sana kuwa na familia ila ndio hivyo tena Mungu anakuwa bado hajaamua.

Walimwengu punguzeni maswali, umeoa? umeolewa? una watoto wangapi? umri unaenda ujue.

Mungu ndio mpanga wa yote.
 
Point sana

Kuna watu wanatamani sana kuwa na familia ila ndio hivyo tena Mungu anakuwa bado hajaamua.

Walimwengu punguzeni maswali, umeoa? umeolewa? una watoto wangapi? umri unaenda ujue.

Mungu ndio mpanga wa yote.

Your points are well taken.

Ila.

Mungu ni chaka tu tunalosukumia mambo yote tusiyoyaelewa vizuri.

Hakuna aliyeweza kuthibitisha yupo.

Na pia, imani ya Mungu (Abrahamic) ina uhusiano mkubwa na unyanyapaaji wa watu wasio na watoto.
 
Your points are well taken.

Ila.

Mungu ni chaka tu tunalosukumia mambo yote tusiyoyaelewa vizuri.

Hakuna aliyeweza kuthibitisha yupo.

Na pia, imani ya Mungu (Abrahamic) ina uhusiano mkubwa na unyanyapaaji wa watu wasio na watoto.
Tafadhali ndugu
Fafanua hapo kwenye uhusiano wa hizo Imani na unyanyapaaji wa wasio na watoto......
 
Tafadhali ndugu
Fafanua hapo kwenye uhusiano wa hizo Imani na unyanyapaaji wa wasio na watoto......
Ni hivi,

Dini hizi Abrahamic, zimehimiza kuzaana.

Zimetukuza kuzaana kuwa ni neema.

Zimesema kuzaana ni agizo la Mungu. Zimesema zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia.

Zimeeleza kwamba mti mtini usiozaa matunda umelaaniwa.

Hivyo, usipokuwa na ntoto, kwa mujibu wa dini hizi, kuna mawili.

1. Una uwezo wa kuzaa/kuzalisha, hujataka tu, hivyo umekaidi maagizo ya Mungu ya kuzaliana.

2. Kama huna uwezo wa kuzaa/kuzalisha, kwa namna moja au nyingine umelaaniwa na Mungu kama ule mti mtini usio na matunda.

Hivyo, kwa mujibu wa falsafa za kina za hizi dini, usipokuwa na mtoto ama wewe umekaidi amri ya Mungu, au umelaaniwa na Mungu. Yote majanga.

Dini zina ubingwa wa kuuma na kupuliza ukiziangalia kwa juujuu, na hivyo unaweza kutafuta aya za kupuliza, lakini ukitazama kwa kina dini ndiyo msingi mkubwa wa kunyanyapaa watu wasio na watoto.
 
Vigezo ni viwili tu
1. Upo tayari kuingia kwenye ndoa
If YES, ingia

2 Upo tayari kuwa na watoto
If YES, zaa

Kinyume na hapo usifanye hivyo vitu.
Na usisikilize watu wanaongea nini
100% correct. Shida huanziavkwa wazazi wanaoleta watoto duniani ili hali hawapo tayari. Mtoto akifika 15 years wanazazi hawahudumii tena anaanza kupalangana mwenyewe.
Kama ni wa kiume hadi akajipate inaweza mchukua muda ndio afikiri kuoa ila kama ataamua kuo kabla ajipate maana yake anaendeleza makosa ya wazazi wake na anaendeleza ukoo ule ule usio na mbele wa nyuma. Kama wa kike ndio utakuta kabint ka watu kanaanza kuchukulia mahusiano mtaji. Kakipata kijana ni mizinga tu kumbe maskini mzazi wake hakapi mahitaji yake, kijana nae hajajipata mwisho anaona isiwe tabu anapita kushoto.
Kakipata mimba kwenye maisha hayo ndio single mama mwingine in town
 
Back
Top Bottom