Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MASJID RAWDHA NA SOKO MJINGA KISUTU
Masjid Rawdha ni huo msikiti kushoto ambao zamani ulikuwa ukijulikana kama Masjid Badawy na hili ndilo jina nililolikuta mimi wakati napata akili.
Kulia ni soko maarufu likijulikana kama Soko Mjinga.
Majengo yote hayo yamebadilika kwa kuvunjwa yale ya zamani na kujengwa mapya.
Hii barabara haikuwa hivi.
Nina picha nilipiga Mnazi Mmoja na nyuma yangu inaonekana barabara hii wakati huo ni barabara ya vumbi.
Nyuma ya barabara hii katika hiyo picha ya mwaka wa 1966 ni barabara ya kupita na kupishana gari moja utaona vibanda vya Soko Mjinga. Barabara hii sasa inajulikana kana Bi. Titi Street.
Leo mchana nimepita hapo nikitokea Mtaa wa Mkunguni na ilipowaka taa nyekundu nimetoa simu yangu na kwa haraka nikapiga picha hii.
Nyuma yangu kwenye makutano ya Lumumba Avenue na Mtaa wa Mkunguni kulikuwa na mti unaitwa Sycamore.
Barabara hii ya Lumumba nayo halikadhalika ilikuwa nai barabara moja na kwenye kona upande wa pili katika miaka ya 1960 ilikuwa barza ya vijana maarufu kwa jina la ''Jobless.''
Turudi kwenye Masjid Rawdha.
Muonekano wa majengo haya mawili kwa pamoja ulinishtua kwani nilikuwa bado sijaliona Soko la Kisutu toka lifunguliwe.
Haraka fikra zangu zikarudi nyuma miaka mingi wakati Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akidarsisha hapo hata uhuru bado.
Hii ilikuwa miaka ambayo Shariff Hussein Badawy alikuwa hapo akisomesha vijana usomaji wa Qur'an kwa njia ya tajwid.
Akili yangu ilituama mwaka wa 1963 Mfungo Sita kama huu tulionao hivi sasa Maulid yanasomwa hapo jirani ya msikiti Viwanja Vya Mnazi Mmoja.
Maulid yale yalileta matatizo makubwa yaliyoishia Shariff Hussein kufukuzwa Tanganyika na kurudishwa kwao Kenya.
Mwalimu wangu Mzee Kissinger kwa jicho lake akiwa kasimama Soko Mjinga aliwaona maofisa wawili wa uhamiaji Wazungu wakiingia msikitini na viatu kutoa notisi ya kufukuzwa nchini Shariff Hussein na ndugu yake Mwinyibaba.
Miaka ile wote wawili vijana wadogo.
Chini ya kila paa hukosi historia.
Hiyo picha ya pili ni mimi nimesimama Viwanja Vya Mnazi Mmoja na nyuma yangu ni barabara iliyokuja kupewa jina la Bi. Titi Mohamed na ukivuka hiyo barabara ndiyo Soko Mjinga.
Hii ilikuwa 1966.
Hebu angalia picha hizi mbili kwa utulivu.
Picha ya tatu ni ya miaka hiyo Shariff Hussein Badawy akiwa na Sheikh Ismail Mohamed mmoja wa wanafunzi wake.