Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla

Ungeficha upumbavu wako ungejitendea haki,
Sijakwambia kuwa kila afukuzwaye na simba huokota almasi!!!!
Bali bahati hubebwa na matukio kwenye muda husika!!
Mamaye daimond hangepata ruhusa kwa mumewe kumpeleka mwanae kwenye matamasha ya watoto kama unavyodai, hivyo pengine angekuwa chokoraa tu kitaani!!!
 
Mungu aliyekuumba amemkosea mara ngapi na Mungu anasamehe,.. Iweje Diamond asimsamehe Baba yake kwa kipindi chote hiko huku akiendelea kujiita Nasib ABDUL? Hii sio sawa kabisa, Mungu hapendi.
 

Acha kutetea ujinga, angemzuia diamond kivipi wakati alimlea Queen Darleen na akawa mwanamuziki hata kabla ya Diamond???
 
watu walivyo wajinga wanasupport atapata laana ! kama kukataana baba na mtoto ni laana mzee laana yake tayari! hivi mtoto wake ni huyu mmoja tu? haters& visevesa atafune mihogo kama.naseeb walivyotafuta zamani
 
Kwani watu wote wamezaliwa na manii za huyo Abdul?kwa akili ya kuvukia barabara tu hiyo ni kiki ya biashara kwa hiyo Hospital wanatumia njaa zake kujitangaza!shule mlienda kusomea ujinga?
 
Huyo dokta anajitangaza kupitia mgongo wa baba Diamond
Ila huyu bwana kaungua siku nyingi sana,aachane na Diamond dawa zipo bure tu zahanati za serikali
 
Nakuchukia diamond kwa hili, baba yangu ametangulia mbele za haki lakini aliyoyafanya hapa duniani kwa mama yañgu yamebakiza donda kwetu na kwa mama, lakini mama hakuwahi kutamka chochote tumesikia pembeni , lakini mapenzi kwa Mzee wetu ni makubwa na tunamlilia kila uchao, unachotakiwa ufahamu wewe nassibu hakuna mkamilifu chini ya jua. Kama makosa tunayomfanyia Muumba wetu angekuwa hasamei tungekuwa wapi sasa? Akili za kuambiwa changanya na zako, hao wanaokushika masikio siku ya hukumu hawatakuwa na wewe
 
i would put a 'like' button a million times for this comment!Mfano mzuri kabisa kwa kanumba!Ila Mungu ndo mwenye kutoa hukumu ya mwisho!WHO ARE WE TO JUDGE.
 
wanaume na nyie mjifundishe somo hapa;
mnatuachia watoto MUNGU akiwasaidia
mnaanza kufanya shoo kwenye hospital;
shauri zenu bhana.
Kipenzi hujambo lakini? umepotea kama shilingi ya mkoloni? nime ku miss sana upo lakini? Anavyofanya Diamond ni kosa lazima amhudumie baba mzazi. Baba yako ni baba tu ahata kam ni Mwenda wazimu ni baba tu. Diamond amekuw ana pesa sasa anamdharau baba yake kwanini? hata kama baba yake ameachana na mama yake yeye Diamond haimhusu ugomvi wa mama na baba mtoto haruhusiwi kuingilia.
 
wanaume na nyie mjifundishe somo hapa;
mnatuachia watoto MUNGU akiwasaidia
mnaanza kufanya shoo kwenye hospital;
shauri zenu bhana.
Ni juzi tu nimesikiliza kipindi redioni Dada mmoja alikuwa anasimulia mazila yake, jinsi alivyopewa mimba na jamaa...alafu jamaa akakimbia....alipogundua anapoishi akamfuata....ndio jamaa eti akafunga mlango wa chumba, akachukua kisu na kumwambia 'si nakwambia utoe hutaki, sasa leo naitoa....baada ya sekeseke dada wa watu akajiondokea na leo anaishi kivyake na mtoto wake wanabangaiza.

Sasa kesho na keshokutwa Mtoto akija kuwa mtu fulani ndio Baba atataka kuja na kukenua meno 'mwanangu'
 
Diamond hii laana haita kupita mpaka umuombe msamaha huyu mzee!
Kwa bahati mbaya laana ya baba ambaye hajakulea, hajui ulikua unakula nini utotoni haikupati..! Otherwise wengi tungekua dampo muda huu. Mungu wa ajabu sana.!
 
Alafu mbona muonekano wake ni wa 'kiborn town' zaidi!? Nawaza tu maana haya mambo ya familia yana tabia za kujirudia sasa mbele ya safari historia isije kusomeka hivi.
 
Unashiriki tendo la ndoa na mwanamke kisha unamwachia mzigo wa kulea mtoto tangu utotoni hadi ukubwani, anahangaika weeeeee.....Mungu si athunani anafanikiwa kimaisha, linajitokeza jinga jinga flani linaanza oooh huyu ni mwanangu. Shit!!!!!!!!ulikuwa wapi siku zote? Siwapendi wanaume woooote wenye tabia hii
 

Iwe iwavyo lakini tuna kitu cha kujifunza hapa! Haya maisha yana siri kubwa sana.
 
Kwa baba ama Kwa mtoto?
Hata sisi wote! mimi sitaki kumuhukumu Diamond wala Baba yake, sababu na kuna cha ufa baina yao wanazijua wao, ila sisi wengine tutafakari na tujipime tungefanya nini kama hali hii ingetukuta sisi? Je ningefunga macho, masikio na mdomo na kupandisha vioo tukanyamaza au tungejiongeza tukasamehe na kusonga mbele?! Maana No situation is parmanent; leo Diamond yuko hivi, rich and famous! je kesho tunajua Diamond atakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…