Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla

Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla

Ijumaa kweli fundi hapa wanatafuta namna ya kumtangaza hyu Dr hamna chochote Dr mwenyewe ana mkataba na Risasi kuandika makala afu hyo hyo Dr ndo anahusika na matibabu ya mzee Abdul
Hapa hamna mgonjwa na kiki tu wanatafuta kumtangaza Dr Shame on you
 
Ur on an emergency to the hospital escorted by the camera crew , this looks so dramatising .. The Kick [emoji122][emoji122] kudos [emoji991][emoji991][emoji991][emoji991]
 
Docta kajitangaza kijanja
Sioni ethics za udaktari hapa
Hakuna kitanda maalum cha kumfanyia mgonjwa uchunguzi
Glove imevaliwa mkono mmoja [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mwandishi/waandishi kuruhusiwa kuingia mpaka ndani ya chumba cha matibabu
Licha ya tukio zima kuonyesha wazi ni la kuandaa lakini walioliandaa daktari mgonjwa na waandishi kwa ufinyu wao mdogo wa akili kwa kukosa weledi (kudhalilisha tasnia ya udaktari )na hata uelewa wao wamekosa kabisa kutengeneza uhalisia wa tukio
Mgonjwa ni kanjanja
Daktari ni kanjanja
Mwandishi ni kanjanja
Na hata gazeti lenyewe ni kanjanja (inafika mahali unaona ni afadhali usome hata uhuru kuliko haya magazeti ya udaku)
 
Kwa yeyote mdadisi, ni rahisi kugundua kwamba huyo mama wa diamond aliandaliwa kwamba achukuliwe picha huku akionekana kusaidiwa na wahudumu wa hapo hospital, ili kijana apakaziwe na magazeti ya udaku.
Alafu... iweje mzee aende kwenye matibabu huku akiwa amejiandaa na wapiga picha?
Alafu.... kama mzee alikwenda kupata matibabu, kwanini aliwaita makanjanja wa magazeti ya udaku ili wakipake kwa mwanae?
Agghhhh....[emoji51] [emoji51] [emoji51]
Halafu hiyo hospital ni jipu
Umeona hapo mapokezi?
Angalia mhudumu mmoja kavaa makubazi
Halafu huko ndani chumba cha daktari, daktari kapiga picha na mgonjwa wake kwenye pozi la kuandaa
Maelezo ya mgonjwa kuwa katumiwa pesa ya tax na daktari kisha akamtibu bure?
Wewe daktari umewasaidia wangapi kwa mtindo huu?njaa mbaya sana
 
Mgonjwa serious kabisa unaenda kwa Dr wa tiba asilia, yaani mtu hali mbaya kabisa kabisa unaenda kwa Dr huyo, alafu huyu mzee msanii kwanza hajatubu Kutoka moyoni mwake na hata magazeti wanamtumia ili kuuza habari zake, cha pili mzee chapombe bado anasa anazipenda. Alafu hata mm kama angekuwa baba yangu kwa staili hii sizani kama ningemsamehe, hapo nina uhakika asilimia mia global publisher wamempa ela na huyo Dr nae kampa ela kwa ajili ya kutangaza hiapitali yake lkn mgonjwa mimi hapo simuoni mzee huyu. Wangeniambia muhimbili, Amana, mwananyamala, kairuki lkn kwa hawa wezi hawa matabibu wa dawa asilia mtu anaenda Kusaga mikokwa ya maembe kesho anakuambia dawa hebu mzee kama anataka msamaha aache drama hizi zinamuaharibia.
 
Kama Mungu tunamkosea anatusamehe 7*70 naye ndiye aliyetuumba. Inakuwaje huyu Mondi kuona kosa alilofanya baba yake ni kubwa kiasi kwamba hawezi kumsamehe? Kama mtoto alipaswa kutambua hawezi pata baba mwingine zaidi ya huyo. Na asisubiri afe ndo aende kwenye msiba kwa mbwembwe. Namkubali Mondi ila kwa hili hapana.
Fuatilia habari za huyo mzee kwenye magazeti na tv za udaku utabadili mtazamo wako
Ishu ya ugonjwa si jambo la maskhara hata kidogo...! Ukifika pale Muhimbili au ocean road utapata picha kamili
Hivi mtu mgonjwa kweli anayeumwa hasa anaweza kupata muda wa kukaa na kupigwa picha za kujiandaa?
 
Naona jamaa kaamua kutembelea mgongo wa Diamond Platnumz kutangaza biashara yake,
 

Abdul Juma ‘Baba D’


Erick Evarist na Gladness mallya

DAR ES SALAAM: Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA


Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.



….Akiwa mapokezi.


CHANZO CHAVUJISHA

Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI

“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA

Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.



ASAIDIWA NA WAHUDUMU

Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU

Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.



VIPIMO VINGINE

Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA

Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.

“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”



NGOZI IMEATHIRIKA

“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.



Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond.


AMWAGA SHUKRANI

Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.



“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.

“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.

Diamond

DIAMOND ANASEMAJE?

Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.



TUMEFIKAJE HAPA?

Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”

chanzo.Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!
Kumbe
 
Shigingo nu noomaa. Yani story inaandaliwa kama movie. Eti Dr. alituma hela ya niniii!!??

Dahh... Na litauza kweli hili.
 
Watoto msipende kuwasikiliza sana mama zenu hamuwezi jua nini kiliwatenganisha.....ni bora tu mondi ajitoe ufahamu amsaidie alafu huyu mzee malipo yake yawe kwa mungu.mwenyewe kwani yeye ndiye anayejua
Mwangalieni kanumba Naye alikuwa na kisasi kama mondi tu
LAKINI hata yeye alikufa na akamwacha baba yake na kinyongo chake moyoni...jiulizeniiii

anayemsikiliza mama ni mtoto mdogo ndugu! yule naye anamiliki mmama mwingine anayiakili yakupima na kuchuja mwenyewe mazuri anayaona mabaya anayaona! rafiki wa kweli na mbaya anamjua bana yake angekuwa rafiki wa kweli wasingefikia hapo.
 
Kwani uyu mzee mtoto wake mi diamond tu. Kwann wasiandike baba wa Queen Dareen azidiwa. Wababa wanajitenga sana na watoto n Mungu hua wa ajabu watoto wa kutengwa hua wanafanikiwa mno. Hlf baadae wana play kua ni victim.
Ugua pole mzee lkn huo ni uchonganishi wa kwenda na waandshi wa habari hosptalini km sio kutaka kumchafulia Diamond ni nn.
Mwenyewe nashangaa[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Kama Mungu tunamkosea anatusamehe 7*70 naye ndiye aliyetuumba. Inakuwaje huyu Mondi kuona kosa alilofanya baba yake ni kubwa kiasi kwamba hawezi kumsamehe? Kama mtoto alipaswa kutambua hawezi pata baba mwingine zaidi ya huyo. Na asisubiri afe ndo aende kwenye msiba kwa mbwembwe. Namkubali Mondi ila kwa hili hapana.
Tatizo sio kusamehe, tatizo lipo kwenye kusahau. Kusahau uliyotendewa ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom