Maskini Dokta Shika ugonjwa umechachamaa pesa hana

Maskini Dokta Shika ugonjwa umechachamaa pesa hana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Dr Louis Shika ana matatizo ya figo kitaalamu tunanaita chronic renal failure stage 5(CKD5HD), alifanyiwa Dialysis Bugando lakini haikuendelea kutokana na upungufu wa pesa, hali ya Dr Shika sio nzuri anahitaji msaada kwa matibabu zaidi juu ya tatizo lake.

Kwa sasa hivi yuko mwanza amelazwa na inaonekana hana matumaini tena hata ndugu hawana matumani.. Kwa kawaida dialysis ama Huduma ya kusafisha figo inagharimu kiasi cha milioni 50 hadi mia kwa mwaka.. Wagonjwa Wa dialysis husafishwa damu kwa muda usiopungua masaa 4 mara tatu kwa wiki kwa maisha yake yote.

Watanzania naombeni tumsaidie sana huyu Mzee wetu ili apate faraja ya uhai tena,kwani asipoendelea kupata huduma ya dialysis basi siku zake za kuishi zitapungua sana.
 
.
Screenshot_20200717-103716.jpg
 
Poleeeh zake sana, Jah amfanyie wepesi na kurudisha hali yake sawa ktk afya njema.
 
nikisikia mgonjwa figo mwenye umri uliokwenda kama Dr. Shika amefikia stage ya kufanyiwa dialysis ki ukweli chance yake ya ku- 'survive' inakuwa ndogo …………………...Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi
 
Daah Mungu amfanyie wepesi...fomu amechukuliwa na nani??

Everyday is Saturday......................... 😎
 
nikisikia mgonjwa figo mwenye umri uliokwenda kama Dr. Shika amefikia stage ya kufanyiwa dialysis ki ukweli chance yake ya ku- 'survive' inakuwa ndogo …………………...Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi
Magonjwa ya viungo vya ndani ya mwili hata kwa umri mdogo ni mtihani sana!! Figo Failure Stage 5 maana yake haifanyi kazi kabisa na kuweka nyingine price yake sio ya kitoto.
 
Pole sana kwake mzee wa itapendeza.,,,,,,,Majuzi nimeona ametia nia nadhani ccm wamekusanya sn pesa za walalahoi waliokosa matumaini ya ajira na kutaka kuingia kwenye siasa....ccm wamekusanya km 5bil basi wamkumbuke huyu ndugu kwani 100mil kwa mwaka na ccm kitu gani.

Huu ujumbe ,mwenyekiti, makamu, katibu mkuu, mwenezi wote wameuona ila watakaa kimya hapo ndipo utaelewa ccm ya wanyonge
 
Dialysis sio mchezo kama huna pesa you are Gone. Kina jamaa zangu mama yao alikuwa na hilo tatizo uzuri walikuwa na pesa waliinunua hiyo machine akawa anafanyiwa na madaktari nyumbani. Kuna siku ilitokea issue ya clotting mechanism kugoma ilibidi akodiwe ndege haraka kupelekwa Nairobi Kenya.
Usiombe hiyo kitu haswa wale wapiga faru John nk
 
Back
Top Bottom