Maskini Saida Karoli


Nashahadia usemi owongo, nakumbuka hili tukio, nilikua na mie naangalia kwenye tv, na nikashangazwa sana. Jamani, acheni tusomesome tu, tuondoe ujinga!
 
Anguko la Saida wala sio Ruge bali ni Felician Mutta. Kwa hivi sasa kitambo anaishi New York USA na familia yake.

Nafikiri waliompoteza Saida ni wapambe na wanafiki wa pembeni kwani ndo waliomshawishi aachane na mzee Muta pasipo kumuonyesha njia mpya ya kupita.

Kumbuka Saida hakuwa na elimu yoyote Mzee Muta kamuokota bukoba kwenye mkesha wa Nanenane mwaka 2000 pale uwanjani Kaitaba. Kumbuka wakati huo Saida alikua akiimba kwenye vilabu vya pombe na maharusi ya watu.Kamleta mjini kwa mara ya kwanza akiwa hajui hili wala lile... pale suala la kudhulumiwa lilikua haliepukiki, muhimu angetulia kuangalia wapi kuna makosa na kurekebisha na bos wake kwa njia za kidipromasia mwishowe wakachapa mzigo.

Lakini kama mjuavyo kawaida ya wapambe. Wanakuchochea ili ukisanue, kikishanuka nao wanaingia mitini. Kama ilivyo ada, masiki hutakiwi kununa au tuseme tajiri hanuniwi. Muta kabwaga na ndo ukawa mwisho wa saida.

Sasa kipi kilikua bora kati ya kupata kidogo na kukosa kabisa???? Je wangekaa kifamilia unafikiri zile kasoro zisingerekebishika? Lakini mkaona mchochee moto ili ukuni uzidi kuteketea...

Aina hizo za wapambe nuksi ndo zimejaa hata humu jf... kutwa kulalamika na kutukana pasipo kutoa mwongozo kana kwamba wao ndo wakamilifu na hawakosea(gi).
 

hivi na marehemu ngurumo nani alikuwa anamuibia.

wasanii wengi wa bongo ni wajinga upande wa nidhamu ya pesa
 
Felician Mutta yule meneja wake wa kwanza sasa hivi sasa yuko wapi?
 
Mutta yupo,nasikia hata studio yake ya FM alishindwa kuiendesha hivyo akatimua wafanyakazi na kuihamishia nyumbani kwake ambapo sasa hivi anafanya na mwanaye pamoja na jamaa kutoka marekani.
 
Nashahadia usemi owongo, nakumbuka hili tukio, nilikua na mie naangalia kwenye tv, na nikashangazwa sana. Jamani, acheni tusomesome tu, tuondoe ujinga!

Lakini alichokisema Mutta kilikuwa ni kweli,wasanii wa Tanzania huwa wakiuza Album wanauza HakiMiliki zao kabisaa,so Obviously Saida kufulia hakuepukiki
 
Saida Karoli hajaibiwa kivile na mtu yeyote
Wapambe ndio walio mrostisha aachane na Muta anamuibia kisha wakampeleka uganda akapiga show watu wakavuta mapene wakasepa
Huo ndio ukawa mwanzo wa mwisho wake

Sasa karudi bukoba anaendelea na shughuli zake alizokua anafanya kabla Muta hajamchukua na kumleta mjini
 

Tena mbaba wa watu aliwahi kumpeleka mpaka kozi ya kiswahili, alipoerevuka akadanganywa kuvunja mkataba wakati huo mpaka gari kale ka toyota mark ii kapewa na Mutta huyohuyo.
 

Ama kweli watanzania tunakulana wenyewe kwa wenyewe! So sad!
 
Mutta yupo,nasikia hata studio yake ya FM alishindwa kuiendesha hivyo akatimua wafanyakazi na kuihamishia nyumbani kwake ambapo sasa hivi anafanya na mwanaye pamoja na jamaa kutoka marekani.

Du kumbe naye kafulia!
 
Tena mbaba wa watu aliwahi kumpeleka mpaka kozi ya kiswahili, alipoerevuka akadanganywa kuvunja mkataba wakati huo mpaka gari kale ka toyota mark ii kapewa na Mutta huyohuyo.

Lakini kamtumia kama daraja. very bad!
 

Soooo unfair jamani.
Nimetamani kujua alipo sasa!
 
Hyo aliyemdhulumu
Mwisho wake atashangaa, dhuluma mbaya

Ameokoka anasali Mlima wa moto kwa Dr,Mh,mchungaji mama...,lakini wa Silent Inn ni Fred Rwegasira na yule wa Kalori ni Felician Mutta alikuwa aliyekuwa mmiliki wa maduka ya kuuza kanda enzi hizo maarufu kwa jina la FM,pia aliwahi kuwa na bendi pinzani ya Wana ikibinda nkoi ,Diamondo ikiitwa FM international akina El Saadat kama sijakosea
 
Nasikia ameokoka Huyo MTU. Kama sijakosea ni Felician Muta.

Aliyeokoka ni Fred Rwegasira wa Bana ikibina Nkoi Daimondo soundo waliokuwa pale Silent Inn kuna wakati akifurahi alikuwa akiwamwagia mapesa wanamuziki wake huku akipiga tumba,enzi zile alikuwa Rugemalila mdogo,,Felician Muta naye akaanzisha bendi yake FM International (Ngwasuma) pia alikuwa na maduka ya kuuza kanda FM ,sasa naye alikuwa anatesa na Kalori akamchambua kama karanga dada wa watu na sasa hana Ee wala Bee anajikimu kwa kupiga ngoma kwenye vilabu vya wanzuki,Wahaya ni nouma,ujuzi wao ni kupiga madili ya pesa ndefu,sasa anasali kanisa la Mlima Wa Moto kwa Dr,mhe,Mchungaji,mama Lwaka
 

Hahahaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…