Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

kwani lazima afanye mziki usio na faida?
 
Mkuu sijawahi kulike comments zako ila kwa hapa nimekubali sema nachukizwa na ule upande wako mwingine
 
Mamaaaaaa [emoji37][emoji37][emoji37][emoji37] imeshakula kwake huyo Rubby dah
Ruby kachemka sana bado ni msanii mchanga hasijifananishe na jide bado hana nguvu ya kutunishiana misuli na media,
Mwaka juzi diamond aliwagomea east africa wakampiga ban wakawa hawachezi nyimbo zake kwenye radio na tv wala hawatoi habari zake lakini bado diamond hakushuka kimusic tayari ana mashabiki wengi sana.
Ruby bado sana
kwani lazima afanye mziki usio na faida?
 
Kwa hiyo Ruby ndo anajua maslahi kuliko Joh Makini au Fid Q?

Au yeye pekee ndiye angelipwa kidogo kuliko wengine?

Hilo buzi linalompa jeuri likimtema ataenda kuomba msamaha tu.

Kibongo kufanya kazi na Clouds ni maslahi tosha hata kama ni bure,Kuna vijana wanavipaji unique lakini wanaishia kuwaimbia wenza wao maghettoni kisa hakuna promo.

Jide mwenyewe akipata nafasi ya pili kukutana na Clouds kwa mara ya kwanza hawezi kushupaza shingo.

Huu mgogoro umemuathiri sema ndiyo hivyo tena.
 
nawashangaa watu mnamsuport ruby wakt hamjui mkataba wake yy na clouds ngja 2xubr ndo mtajua wasanii wengi bongo hawajaenda shule walienda xul,mikataba bdo inawasumbua
 
mbona kila siku ijumaa nilikuwa namuona diamond east africa ile wkend show? acha uongo wewe
 
Hapo kwenye "wengine" kina nani mm ninavojua kila MTU Ana mkataba wake wa malipo sasa Kama ruby kaambiwa laki 5 ni yeye ila usituaminishe kwamba na kina weusi, fid Q wanalipwa 5
Vipi mbona umepanic sana... Siasa za fiesta zisikie mtaani tu wewe kama unawapenda clouds ni shabiki yao nenda kawasapoti upate burudani.. Ila siasa zao ni ngumu aliyezifaulu ni AY, Jide na Diamond Platinumz wengine wamezishindwa ata Ruby atashindwa maana ata mbishi Sugu aliuza timu dakika za majeruhi.. Usipoteze nguvu zako bure hapa.
 
Nyie mnaosema kuhusu Diamond, hakuna media inayomuweza tena Diamond hapa East Africa.. Hao Clouds wamemshindwa na wengine wamemshindwa.. Diamond ana nguvu kuliko.
 
Wabongo tunaogopa sana kupambana, naamini akikomaa atafanikiwa tu ..EFM ipo na ni mbadala wa hiyo redio yenu mnaotaka iabudiwe...mnatakiwa kuumpa moyo Ruby ili asimamie anachokiamini

Redio ya mkoa mmoja kwa msanii mwenye malengo ya kutoboa BET itamsaidia nini?

Unadhani watz wangapi husikiliza online au kupitia madish yao luningani?
 
Wanarukaruka jukwaan kama vyura alaf pesa ya kimaaandaaaaaaazi...

Ndo mana naona hata diamond hayupo .. Cjui kwa mikoa mingine...
 
na huyo diamond hata Leo clouds wakimtaka kumtumia wanamtumia japo hawezi lipwa km anavyolipwa young killer au ruby Ila hawamlipi 50mils per show!!never!!!
Katika watu walioamua kumharibia Ruby ni hawa walio mshauri kukataa hiyo show halafu haitoshi kwenda kwenye social media kujidai ana tunisha misuli.

Ruby alitakiwa kupiga hiyo show halafu ange malizana nao na bila shaka kuna sababu walizo ziona Ruby alitakiwa alipwe hiyo Laki tano.

Mbona kuna wasanii hawajapata show kabisa? Halafu Ruby alitakiwa kupiga hiyo show kama shukrani kwao tuu kwa kumsaidia kumtoa maana nasikia mwaka jana ilibdi azunguke fiesta zote bure maana ndio zawadi aliyo ahidiwa ikiwa kama kumtangaza..

Ruby hajafikia level ya kuonekana ana nyanyaswa au kunyonywa kabisa Ruby ni msanii mchanga na biashara za wasanii wachanga ndivyo zilivyo..

Kama kuna mtu anataka kufananisha misuli ya Jaydee na Ruby basi kichwani hayuko sawa.. Kama kuna mtu anataka kufananisha stuation hii ya Ruby na ya Jaydee basi anapaswa kupimwa akili.

Kwanza Ruby hajatumiwa kwa vyovyote vile na Clouds kutengeneza faida yeyote ile kwa hiyo kwa vyovyote vile Ruby hatakuwa na hoja.. Maana bila shaka Clouds wana hoja za kutaka kumlipa laki tano.

Halafu kama alikuwa hakubali hiyo offer ange kataa halafu akapiga kimya au ange angalia faida ya kukubali hiyo offer ukiacha pesa... Si kila kitu lazima kikulipe papo hapo hata Jide hizo za bure alizipiga sana? Ruby ana muda gani kwenye muziki?

Tanzania tuna media house zenye nguvu tatu tuu kwa sasa.. CLOUDS , IPP NA EFM .
Msanii akigombana na moja kati ya hizo nguvu yake hupungua.. Kinyume awe na jeuri, nguvu, kiburi, katili kama Lady Jaydee..

Unajua wengi wakiona Lady Jaydee kaweza wanadhani ni rahisi.. Hahahaha.. Huyu Jaydee huwa namuangalia mara mbili si mmalizi hakika sijawai ona mwanamke wa namna hiyo sidhani kama Ruby ataweza.

Halafu ukiaacha swala la Clouds ni wazi Ruby ana shida kidogo nadhani kuna maswala yake hayako sawa.. Sidhani kama saikolojia yake kama iko sawa.... Maana hivi karibuni amekuwa akilalamikiwa sana na watu kuwa amekuwa hatokei kwenye shooting na mambo mengine..
 
Nako 2 Nako nawamis sana, hasa pale kwenye mstari wao, alie kupandisha ndio atakae kushusha.. Aha haa Nako 2 Nako.. Wapi baba Ray c! Maisha marefu kwenu maninja wangu.
 
Sasa mkuu ukisema hivo ina maana hata bongo kusiwe na wapinzani kwa kuwa hata kina lowassa, mrema walishndwa
Clouds wanatakiwa wapingwe kwa namna yyte
Japo najua kupingana nao ndio mziki ulipo, ila anapo tokea mtu ana sema ukweli mi namsapot
 
mbona kila siku ijumaa nilikuwa namuona diamond east africa ile wkend show? acha uongo wewe
Acha lubisha kama hujui kitu diamond na east africa walipatanishwa mwezi wa 5 baada ya kikao baina yao mwaka jana yote hawakupiga nyimbo za diamond
Walianza kupiga mwezi wa 5 baada ya kupatana, wakina harmonize walikuwa wanaenda kufanya interview hawakuruhusiwa kumtaja diamond
 
yasije mkuta kama ya wale mapacha na harakati zao za vinenga mwisho wa siku tukawaona syo wanaharakati walioojisalimisha mjengoni clouds
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…