Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Naomba mtu mmoja mtaalamu wa hesabu na anayejua haya mambo kwa uweledi atupigie hesabu, mbunge mmoja kwa mwaka mmoja wa kusinzia (kwa wanaosinzia) Bungeni anapata kiasi gani??? Na kwa idadi ya wabunge wote inatumika kiasi gani? Na je sitting allowance ya kamati wanalipwa? Kama ndiyo je ni kiasi gani?Maslahi ya MBUNGE wa Tanzania by Martin Maranja Masese
Mshahara & Posho — Sh16.5M (mwezi)
Posho kujikimu — Sh250,000 (siku)
Posho kitako — Sh220,000 (siku)
Kiinua mgongo — Sh272M (5yrs)
Mkopo gari — Sh90M (5yrs)
Mfuko wa Jimbo — Sh55M (mwaka)
Malipo ya mafuta, katibu na dereva Posho
ziara za mafunzo ughaibuni
Posho za vikao kamati & semina
Mkopo mkubwa – dhamana ubunge
Bima ya afya kwa familia, BURE
Passport hadhi ya kibalozi, BURE
Mshahara hauna makato yoyote.
Hakuna makato mifuko hifadhi ya jamii
View attachment 3231790
Tukijua hizi hesabu tutapata hasira za kuwawajibisha wabunge wetu wakatatue kweli kero zetu au kutusemea bungeni. Lakini pia tutakua na nguvu ya kuchagua wawikilishi sahihi...
Na je wawakilishi toka Zanzibar (Baraza la wawakilishi) nao wapo Bungeni? Kama ndiyo, je wanalipwa mara mbili?
NB: KAMA HII HABARI NI YA KWELI