Masogange alipohojiwa na gazeti la mtanzania alikuwa na haya ya kusema;"Kwanza mimi nimeokoka, halafu huyo Makonda hata sijawahi kuonana naye ana kwa ana zaidi ya kumuona kwenye vyombo vya habari, mimi nataka wanaonishutuhumu waache kukurupuka wao wanapokutwa na tatizo waangalie njia ya kujinasua na si kusingizia wengine"
"Wamekurupuka na wananituhumu kwa kitu ambacho hawakifahamu, asimuhukumu mtu kwa historia mimi nishaokoka nina miaka mitatu sasa niko hapa nchini nafanya kazi zangu za halali,
hakuna asiyejua na sipendi kabisa kujihusisha na makundi yoyote yale kwa kuwa hawajui undani wa maisha yangu sasa wanaanza kuzusha na kuhusu uhusiano na mkuu wa mkoa, sidhani kama hata tuliwahi kuonana macho kwa macho, mimi namuona kwenye TV na magazeti nadhani na yeye ni hivyohivyo,
Nilishaacha kujihusisha na sanaa na burudani miaka miwili iliyopita sasa"