Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,157
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Masogange mbona mzuri sana tu, na lile zigo mtu anaweza uza kiwanja na makaburi yake....
Hebu kwenda huko....ule peke yako kwani sumu ile....
Mko kama mia hivi....unaowajua na usiowajua.
Na hivi siku nyingi sija'zamiwa' basj kuko ndembendembe
Kwendaaaaaa
Hiv akina Matola na matumbo wapo au wameacha umbea, akina Money Stunna BADILI TABIA Mrembo by Nature Heaven on Earth
Ehh binamu si nilisikia umeokoka na umeacha umbea? Imekuaje akii
Hapo vepe
Mashallah, Wolper angekua hajaacha ile michezo yake nadhani angemtafuta sana huyu!
Uongo tu mimi wala siamini.Davido star wa dunia kakosa watoto wakalia hadi atoke na popoma masogange?
Thou nae ni mkali ila kwa hadhi ya Davido hapana aisee.
Hivi Masogange anajishughulisha na nini huko Sauz?
PENZI ni kikohozi, kulificha huwezi ! Habari ya mjini kwa sasa ni mahaba niue ya muuza nyago kwenye nyimbo za wanamuziki wa Bongo Fleva, Agness Gerald Masogange na staa wa muziki nchini Nigeria Naija , David Adedeji Adeleke Davido baada ya kuoneshana penzi zito hadharani .
Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Masogange aliyeko Johannesburg nchini Afrika Kusini Sauz kimelieleza gazeti hili kwamba, wawili hao kwa sasa ni wapenzi wa kupika na kupakua .
Chanzo hicho kililimwagia gazeti hili ubuyu kwamba , katika tukio la hivi karibuni , Davido ambaye ni staa wa Ngoma za Skelewu na Aye alitokea nchini kwao, Nigeria na kwenda kukutana na mwanadada huyo nchini Afrika Kusini ambako wanaponda raha kwa sasa .
Yaani Masogange na Davido ni mahaba niue, wanaponda raha kwa kwenda mbele maana hata juzi tu walikuwa kwenye klabu moja hivi wanakunywa na kula pamoja huku wakifurahia vilivyo uumbaji wa Mungu .
Davido ametinga hapa Sauz akitokea Nigeria kwa ajili tu ya kuja kukutana na Masogange ambaye mara nyingi anakuwa Sauz, kilisema chanzo hicho.
WANASWA KLABU , WANYWESHANA POMBE
Chanzo hicho kilienda mbele zaidi na kutuma video ambayo inamuonesha Davido akimnywesha pombe Masogange huku wakiwa wamelewa tilalila bila kujali kwamba walikuwa klabu ambako kuna watu wengi.
Angalieni hiyo video kwa ushahidi zaidi, Davido alikuwa akimnywesha pombe kali Masogange na kuna wakati Masogange naye alikuwa akimnywesha Davido .
Nilikuwa nao klabu wakifanyiana vitendo vya kimahaba kama kunyweshana pombe kwenye chupa moja bila kujali macho ya watu , kilidadavua chanzo hicho na kuongeza:
Nakwambia huku ( Sauz ) Masogange na Davido wanakula bata hadi kuku wanaona wivu . Yaani ni mapenzi mazito usiwapimie .
DIAMOND ATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Davido ambaye ni rafiki wa karibu na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond Platnumz inadaiwa ndiye aliyemuunganishia jamaa huyo kwa Masogange kwani alikuwa akimsikia na kumuona kwa muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii na akampenda .
Si bure , kilichomvutia Davido ni ule mzigo wa Masogange ( makalio ) maana kila siku huwa anautundika kwenye Instagram so akaona mtu wa kumpigia pande ni Diamond , kilidai chanzo hicho.
MASOGANGE ATAFUTWA
Baada ya kuzipata habari hizo na ushahidi wa video, gazeti hili lilimtafuta Masogange ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba kutokana na mwanadada huyo kutumiwa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp bila kujibu.
Chanzo: GPL
Habari ya mjini sasa ni Lowasa na Mafuriko,umbeya utarudi 26/10.
Sitowaangusha hahaha
Haaaah me cto shangaa Kama aliweza kutoka na yule msanii na producer techno miles wa Nigeria hata kwa davido haitokuwa maajabu sana