Masogange, Davido ndani ya "PENZI" zito

Masogange, Davido ndani ya "PENZI" zito

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
PENZI ni kikohozi, kulificha huwezi ! Habari ya mjini kwa sasa ni mahaba niue ya muuza nyago kwenye nyimbo za wanamuziki wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange ' na staa wa muziki nchini Nigeria ‘Naija' , David Adedeji Adeleke ‘Davido ' baada ya kuoneshana penzi zito hadharani .

Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Masogange aliyeko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz ' kimelieleza gazeti hili kwamba, wawili hao kwa sasa ni wapenzi wa kupika na kupakua .

Chanzo hicho kililimwagia gazeti hili ‘ubuyu ' kwamba , katika tukio la hivi karibuni , Davido ambaye ni staa wa Ngoma za Skelewu na Aye alitokea nchini kwao, Nigeria na kwenda kukutana na mwanadada huyo nchini Afrika Kusini ambako wanaponda raha kwa sasa .

"Yaani Masogange na Davido ni mahaba niue, wanaponda raha kwa kwenda mbele maana hata juzi tu walikuwa kwenye klabu moja hivi wanakunywa na kula pamoja huku wakifurahia vilivyo uumbaji wa Mungu .

"Davido ametinga hapa Sauz akitokea Nigeria kwa ajili tu ya kuja kukutana na Masogange ambaye mara nyingi anakuwa Sauz, " kilisema chanzo hicho.

WANASWA KLABU , WANYWESHANA POMBE
Chanzo hicho kilienda mbele zaidi na kutuma video ambayo inamuonesha Davido akimnywesha pombe Masogange huku wakiwa wamelewa tilalila bila kujali kwamba walikuwa klabu ambako kuna watu wengi.

"Angalieni hiyo video kwa ushahidi zaidi, Davido alikuwa akimnywesha pombe kali Masogange na kuna wakati Masogange naye alikuwa akimnywesha Davido .

"Nilikuwa nao klabu wakifanyiana vitendo vya kimahaba kama kunyweshana pombe kwenye chupa moja bila kujali macho ya watu ," kilidadavua chanzo hicho na kuongeza:

"Nakwambia huku ( Sauz ) Masogange na Davido wanakula bata hadi kuku wanaona wivu . Yaani ni mapenzi mazito usiwapimie . "

DIAMOND ATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Davido ambaye ni rafiki wa karibu na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz ' inadaiwa ndiye aliyemuunganishia jamaa huyo kwa Masogange kwani alikuwa akimsikia na kumuona kwa muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii na akampenda .

"Si bure , kilichomvutia Davido ni ule mzigo wa Masogange ( makalio ) maana kila siku huwa anautundika kwenye Instagram ‘so ' akaona mtu wa kumpigia pande ni Diamond , " kilidai chanzo hicho.

MASOGANGE ATAFUTWA
Baada ya kuzipata habari hizo na ushahidi wa video, gazeti hili lilimtafuta Masogange ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba kutokana na mwanadada huyo kutumiwa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp bila kujibu.

Chanzo: GPL
 
Uongo tu mimi wala siamini.Davido star wa dunia kakosa watoto wakalia hadi atoke na popoma masogange?
Thou nae ni mkali ila kwa hadhi ya Davido hapana aisee.
 
Labda kajipozisheni pazuri davido kanaswa, ila pale davido hatoki
 
Yule ndo boss wa mtandao wa bure akii

Ha ha ha ha lakn huku mnaijeria kule mbongo hapo wamekutana full fixi ye davido ajue kama wa kupiga tu lakn akileta mahaba Niue itakula kwake
 
huyu ndiyo demu wa davido siyo hlo tipwatipwa lenu!
unnamed1.jpg
 
Masogange ndio nchigani aisee?? Sie tupo bussy na uchaguzi we unaleta mapenz
 
Kwan wa maprado hua anapitiaga mlango ule au kushika tu

Hebu kwenda huko....ule peke yako kwani sumu ile....
Mko kama mia hivi....unaowajua na usiowajua.
Na hivi siku nyingi sija'zamiwa' basj kuko ndembendembe
 
Back
Top Bottom