kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Vijana ni waelewa sana, maana ni walewale walioambiwa hapa ni chooni, hapa ni jikoni, huu ni moto na haya ni maji wakatii hadi leo kuwa hapa ni chooni, hapa ni jikoni na pale ni chumba cha baba na mama tusiingie bila kubisha hodi.
Vijana hawahawa kama kungekuwa na viongozi ambao wangewaambia kuwa hapa panastahili kufanyia biashara na pale hapafai kwa biashara, banda la biashara linatakiwa liwe hivi na lisiwe vile wangejipanga wenyewe. Wangejua wapi panafaa kufanyia biashara na watu wangapi wanatosha kufanyia biashara sehemu husika na banda linatakiwa lifaneneje. Watakaokosa Kariakoo wangehamia Magomeni, watakao kosa nafasi DSM wangehamia wenyewe Kibaha kwenye nafasi, watakaokosa kibaha wangehamia Mlandizi, wtakaokosa mlandizi wangehamia Chalinze na kuendelea kutafuta nafasi hadi Mkata, kwenye Kata yao hadi kijijini kwao, maana huko DSM kumejaa hakuna nafasi ya kufanyia biashara.
Shida kuu ya watawala ni kutoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye majiji wawatafutie vijana wote sehemu ya kufanyia biashara. maagizo haya yanawavutia vijana wengingi kutoka mikoani vijijini kuja mijini maana nafasi za kufanyia biashara hazijai huko zipo zinatafutwa. Matokeo ya maagizo hayo ya kuhakikisha vijana wanapatiwa maeneo ya kufanyia biashara ndiyo yanayosababisha msongomano wa vijana wenye aina tofauti za biashara kusongamana kwenye eneo dogo masokoni, mitaani, na kando ya barabara. Wanajenga mabanda ya mbao laini, nylon, makaratasu na magunia chakavu ambayo ni rahisi sana kushika moto.
Kwenye msongamano huo vijana wanahitaji umeme kwenye mabanda na meza zao kwaajili ya mwanga, kuchaji simu, kuchemsha chai, kutengeneza simu na vifaa vya electronics. Vijana wanajiunganishia umeme kwa nyaya zisizokuwa na ubora na viwango vya kuhimili matumizi wanayohitaji kuyafanya pale.
Kwenye msongamano huo kuna vijana wanahitaji kuwasha moto wa mkaa, kuni na gesi kupikia na kuchomea viazi, mihogo, mahindi, nyama, nk.
Mazingira kama haya yanavutia ajali za moto zitokee kila wakati kwasababu zifuatazo:
1. Ajali kutokana kuunganisha umeme bila utaalam kwenye mabanda ya mbao na mabox
2. Cheche za moto kutoka kwenye mkaa, kuni na gesi wanazopikia kwenye eneo la biashara
3. Kupata fidia. Kuna mtu anatafuta kupata fidia ya hasara kutoka kwa wanasiasa wapenda kura na uongozi baada ya soko kuungua, hivyo anasababisha moto.
4. Kujengewa soko jipya na bora kuliko mabanda yao, hivyo wanalitia moto wajengewe kama wale wenzao waliopata kadhia kama yao.
5. Waliokosa nafasi sokoni. Vijana waliokosa nafasi pale wanaweza kulichoma soko ili wakose wote na likijengwa upya wapate nafasi pia.
View: https://youtu.be/Dl8GGb6WHeo?si=91HrVJHct-m76C5-