Masoko makubwa barani afrika mwanzoni mwa mwaka 2026

Masoko makubwa barani afrika mwanzoni mwa mwaka 2026

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
97
Reaction score
197
Masoko Makubwa ya Afrika Februari 2026.

Mwezi Februari umeonyesha mwanzo mzuri kwa chumi kuu za Afrika mwaka 2026, imechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei, kuimarika kwa sarafu za ndani na kuongezeka kwa hamu ya wawekezaji.

🎯Misri Yakumbwa na Hali Ngumu ya Biashara
Sekta binafsi ya Misri imeonyesha kudorora kwa shughuli za kibiashara kuliko nchi nyingine nane kubwa barani Afrika.
Kiwango cha PMI cha Misri kilishuka hadi 48.9 mwezi Februari kutoka 49.8 mwezi Januari. Alama chini ya 50 inaashiria kudorora.

Uganda iliongoza kwa ukuaji 54.2,ikifuatiwa na Nigeria, Kenya, Msumbiji, na Afrika Kusini. Ghana na Zambia bado zipo kwenye hali ya kusuasua ingawa Ghana inaonyesha dalili za kutengamaa.

🎯Mfumuko wa Bei Unaendelea Kupungua
Nchi nyingi za Afrika zimeanza kurejea kwenye tarakimu moja ya mfumuko wa bei jambo linalotoa ahueni kwa walaji na watunga sera.

Uganda Ina mfumuko wa bei wa chini zaidi 2.9%.
Ghana Imefikia 3.3%, ikisaidiwa na bei kubwa ya dhahabu iliyoimarisha sarafu ya Cedi.
Zimbabwe na Kenya Zimepungua hadi 3.8% na 4.3% mtawalia.
Zambia Ilishuka hadi 7.5%, kiwango cha chini zaidi tangu 2019.

🎯Kwacha ya Zambia Yaongoza Katika Kuimarika kwa Sarafu
Sarafu za Afrika zimeanza kutulia dhidi ya Dola ya Marekani katika miezi miwili ya kwanza ya 2026.
Kwacha ya Zambia Ndiyo sarafu iliyoimarika zaidi kwa 17.7% ikichangiwa na bei nzuri ya shaba.
Naira ya Nigeria Imeimarika kwa 6.95% kufuatia marekebisho ya sera za fedha.

Tanzania na Ghana zimeshuhudia sarafu zao zikishuka thamani kwa 3.99% na 2.60% mtawalia.

🎯Nigeria Yaongoza Katika Masoko ya Hisa
Soko la hisa la Nigeria limekuwa na kasi kubwa zaidi barani Afrika mwaka huu.
Fahirisi yake imepanda kwa 34.4% kwa thamani ya Dola.

Tanzania Inashika nafasi ya pili kwa ukuaji wa 33.4% kutokana na ushiriki mkubwa wa wawekezaji.

Zimbabwe na Ghana Zimefuata katika nafasi za juu kwa kupata faida ya zaidi ya 28%.

🎯Benki Kuu Zaanza Kupunguza Riba
Baada ya miaka kadhaa ya kupandisha riba ili kudhibiti mfumuko wa bei,benki kuu nyingi sasa zimeanza kupunguza viwango hivyo ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Nchi zilizopunguza riba ni Kenya, Misri, Angola, Ghana, Msumbiji, Zambia, Nigeria, na DRC.
Upunguzaji mkubwa ukiwa Ghana ilipunguza kwa asilimia 2.5 hadi 15.5% na DRC hadi 15%.

uku waliobakia palepale Uganda, Afrika Kusini, Tanzania, Namibia, na Zimbabwe.

Rwanda Ndiyo nchi pekee iliyopandisha riba kufikia 7.25%.

🎯Soko la Eurobond Lafunguka Tena
Mataifa ya Afrika yameanza kukopa tena kwenye masoko ya kimataifa kutokana na kuimarika kwa hali ya ukwasi duniani.
Hadi kufikia sasa mwaka 2026, mauzo ya dhamana za serikali yamefikia Dola bilioni 5.95,kiwango cha juu zaidi tangu mwaka 2013.
Kenya iliongoza kwa kutoa Eurobond ya Dola bilioni 2.25.
Mataifa mengine ni pamoja na Ivory Coast, Benin, na Cameroon.
 
Back
Top Bottom