Toosie Slide
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 788
- 955
Ukweli unapigwa pingu ili uongo uzidi kuenea.
Ahsante sana kwa Uzi wako mzuri
..
Ahsante sana kwa Uzi wako mzuri
..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye psychology unaweza ukaona vizuri kwa nini hayo aliyoandika mwandishi yanatokea na kukua zaidi na hata kuweza kufikiriwa kuwa ni ukweli.
Ubongo unaweza kukudanganya ukaona unachokihisi, sikia, gusa, nusa, onja au ona ni kweli au ni uongo au haiwezekani. Hii ni tabia ya ubongo.
Mambo unayofanya mara kwa mara au taarifa inayojirudia rudia mara nyingi, ubongo huweza kukudanganya kuwa ni sahihi, vema; ndio ukweli.
Ukweli hatahivyo, ni kuwa hao wanaotengeneza habari au taarifa zisizo za kweli, ukweli fake wanafahamu kwa kina ubongo ulivyo; ni wanasaikolojia wa hali ya juu.
Katika hili, hao wanaotengeneza ukweli fake wanafahamu jamii. Wanajua wazi kuwa watu wengi duniani wameshajiingiza kwenye mambo ambayo haiwezekani akili kufanya kazi kwao inavyotakiwa.
Kuhusu hii kanuni uliosema ni kweli. Lakini kuna suala la tamaa ya mdaraka, si "utawala" na tamaa ya mali si "utajiri". Haya yote yako kwenye ubongo.Kauli yako Ni kweli kwa asilimia kubwa. Lkn kuna kanuni ya mchepuko (exception rule).
Hadhira iliyo na weledi wa kuhakiki habari inaweza kuzitambua na kuzikataa habari feki. Naongelea information analysis evaluation and verification
Muandishi ni atheist na gay. Anaamini kuhusu evolution ila ni jamaa mwenye akili sana na hachoshi kumsoma.Mwandishi anadai kuwa Biblia ni hadithi za Kutunga, Japo hajatueleza Chanzo cha Maisha kwa falsafa yake. Hapo Kakosea.
Nimekubali ulipomnukuu Hitler kuwa ili kutengeneza propaganda utahitaji kurudia maneno, Hata Kibiblia hii inakubalika inaunda Imani.
Nakubaliana nawewe kwa hili, Mwandishi angefanya uchambuzi yakinifu wa madai yake mfano Uhusiano wa Soda za Coca Cola na Magonjwa. Angechambua pia changamoto za dini (maana amedai ni hadithi)Kauli yako Ni kweli kwa asilimia kubwa. Lkn kuna kanuni ya mchepuko (exception rule).
Hadhira iliyo na weledi wa kuhakiki habari inaweza kuzitambua na kuzikataa habari feki. Naongelea information analysis evaluation and verification
kudai kwako "uchambuzi yakinifu" wa uhusiano kati ya soda za Coca Cola na magonjwa, ni ushahidi mwingine wa dunia inaishi na kuamini ukweli wa kutunga na kubuni.Nakubaliana nawewe kwa hili, Mwandishi angefanya uchambuzi yakinifu wa madai yake mfano Uhusiano wa Soda za Coca Cola na Magonjwa. Angechambua pia changamoto za dini (maana amedai ni hadithi)
Akibainisha pasi na Shaka yoyote kuwa madai yake ni ya Kweli, Weledi wake utadhihirishwa Vinginevyo Yeye ndiyo Katunga hoja zisizo na majibu
Unapokuja na madai ya 'Aina' yoyote unapaswa kuthibitisha pasi na Shaka yoyote, Uhalali wa madai hayo.Mwandishi ameshindwa kama ambavyo wewe pia umeshindwa.kudai kwako "uchambuzi yakinifu" wa uhusiano kati ya soda za Coca Cola na magonjwa, ni ushahidi mwingine wa dunia inaishi na kuamini ukweli wa kutunga na kubuni.
Kuhusu dini, hana cha kuthibitisha (kuwa ni ukweli wa kutunga) kwa kuwa hakuna ushahidi wa kihistoria, sayansi au hata wa kimantiki dhidi ya yasemwayo. Utathibitisha nini apo?
Muandishi ni atheist na gay.
Nakubaliana nawe.Kuhusu hii kanuni uliosema ni kweli. Lakini kuna suala la tamaa ya mdaraka, si "utawala" na tamaa ya mali si "utajiri". Haya yote yako kwenye ubongo.
Watu wengi duniani wanaodhibiti Serikali hawako kwenye hizo nafasi kupitia utaratibu unaotakiwa, ambao kimsingi ndio ukweli halisi.
Kwa sababu hiyo haishangazi kuona ukweli fake ukitawala na kuongoza maisha ya watu.
Hao kwa sababu wanajua wanadhibiti Serikali, kwa mfano kinyume na utaratibu unaotakiwa hawawezi kukubali kanuni ya mchepuko (exceptional rule).
Kanuni hii itaweza kufanya kazi pale jamii itakapo kuwa na uelewa wa kina wa mambo, elimu na maarifa ya vitu.
Mbona umekopy kipande kidogo tu ya niliyoandika? Huo ndiyo upotoshaji wenyewe na si uungwana.Mwandishi anaweza kuwa atheist, theist, au deist.
Pia anaweza kuwa gay, straight au ambivalent.
In each case, what difference would it make as far as his arguments in the book are concerned?
Bado kwenye hiyo asilimia 10 waliopata elimu ya kidato cha nne na kuendelea kama ulivyosema, zaidi ya robo tatu elimu yao ni service education si analysis.Nakubaliana nawe.
Hata viongozi wa dini zetu pendwa za Ukristo na Usilam wanapitia barabara hiyo.
Tanzania ina watu wenye elimu ya kidato cha 4 au zaidi walio chini ya 10%, per UNESCO's data.
Kwa hiyo, watu 90% wanaongozwa na hoja zinazooanzia kwenye hisia badala ya hoja zinazooanzia kwenye mantiki.
Tupanue education attainment level ya nchi angalau kufikia F4 education attainment level ya 51%, na mengine yatafuata.
Hili suala la kuweka umuhimu kwenye alichosema mtu na sio mtu mwenyewe ni dhana nzuri. Wakati mwingine inaleta mkanganyiko. Hata na Yesu aliipigia chapuo. Yafuatwe wanayosema na si walivyoishi na kutenda waandishi! Mtu mwovu unena maovu. Mti tunautambua kwa matunda yake. Mtu awazavyo rohoni mwake ndivyo alivyo. Tunaenenda kwa imani. Tunaishi kulingana na tunavyoamini. Tuaminivyo ndivyo tuishivyo. Imani sio tu katika dini bali ni katika maisha yote ya binadamu.Mwandishi anaweza kuwa atheist, theist, au deist.
Pia anaweza kuwa gay, straight au ambivalent.
In each case, what difference would it make as far as his arguments in the book are concerned?
Umeeleza vema mkuu.Hili suala la kuweka umuhimu kwenye alichosema mtu na sio mtu mwenyewe ni dhana nzuri. Wakati mwingine inaleta mkanganyiko. Hata na Yesu aliipigia chapuo. Yafuatwe wanayosema na si walivyoishi na kutenda waandishi! Mtu mwovu unena maovu. Mti tunautambua kwa matunda yake. Mtu awazavyo rohoni mwake ndivyo alivyo. Tunaenenda kwa imani. Tunaishi kulingana na tunavyoamini. Tuaminivyo ndivyo tuishivyo. Imani sio tu katika dini bali ni katika maisha yote ya binadamu.
Hili suala la kuweka umuhimu kwenye alichosema mtu na sio mtu mwenyewe ni dhana nzuri. Wakati mwingine inaleta mkanganyiko. Hata na Yesu aliipigia chapuo. Yafuatwe wanayosema na si walivyoishi na kutenda waandishi! Mtu mwovu unena maovu. Mti tunautambua kwa matunda yake. Mtu awazavyo rohoni mwake ndivyo alivyo. Tunaenenda kwa imani. Tunaishi kulingana na tunavyoamini. Tuaminivyo ndivyo tuishivyo. Imani sio tu katika dini bali ni katika maisha yote ya binadamu.
Mbona umekopy kipande kidogo tu ya niliyoandika? Huo ndiyo upotoshaji wenyewe na si uungwana.
Najaribu kuhakikisha kuwa kanuni za makabiliano ya kimantiki zinazingatiwa.
Mosi, tunatofautisha mleta hoja na hoja.
Pili, tunatofautisha mleta hoja na rafiki wa mleta hoja.
Tatu, tunakwepa kosa la kimantiki liitwalo genetic fallacy.
Nilipoona bandiko lako, nikafikiri kwamba umekiuka kanuni hizi.
Tatizo zaidi ulitoa tamko bila ithiobati.
Na kama unavyojua, tamko lisilo na vazi la ushahidi hupigwa pingamizi lisilovaa nguo ya ushahidi pia.
Na ikitokea hivyo, makabiliano ya kinatiki huwa yamekufa.
Kwa hiyo, ni muhimu kukubaliana juu ya rules of engagement kabla ya engagement yenyewe.
Nimekuelewa kiasi. Lakini pale yule bwana niliyemjibu alitaka kujua Bwana Noah anaamini nini/ana falsafa gani kuhusu chanzo cha maisha. Ndiyo nikaona nimuambie kuhusu jinsi muandishi alivyo, kwamba ni aetheist na ni shoga (yaani hakubaliani na viwango vya maadili vinavyokubaliwa na watu wengi) anayeamini katika nadharia ya evolution. Mimi sijali kama Noah ni shoga na hapana maana nimesoma vitabu vyake, Homo sapiens na Homo Deus na humo ndimo kuna ushahidi kwamba yeye ni Atheist anayeamini katika nadharia ya evolution.