Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimependa unavyoielewa Biblia. Huko sitavinjari kwa leo. Alichosema mtu ni maneno. Mtu mwenyewe ni matendo. Kwako kuna ukweli mmoja nao ni kuwa matendo ni muhimu kuliko maneno. Je, mtu mwenyewe ni muhimu kuliko alichosema? Swali hili laweza kuwa crude! Nataraji utanielewa. Tutafika wakati tutakuwa na jambo zuri lakini siku tukijua chanzo chake tutagwaya.Umeeleza vema mkuu.
Lakini kuna ukweli mmoja nao ni huu: matendo ni muhimu kuliko maneno.
Ukiwa mtu makini unagundua kuwa masimulizi ya biblia yalikusanywa kwa nyakati mbalimbali na watu mbalimbali.
Biblia kwangu binafsi ni zaidi ya maandishi. Naweza kwa hakika kusema, biblia ndio msingi na kilele cha sayansi.
Katika biblia utakuta nini kinatakiwa na nini hakitakiwi kufuata au kuishi. Hivi viliwi utavikuta kwenye biblia.
Watu walio wengi wanaona katika biblia kuwa chote kilichomo, kilichoandikwa katika vitabu vya biblia ndicho kinachotakiwa kufuatwa. Hili ni kosa.
Kwa wengine kwa sababu kwamba biblia ni Neno la Mungu, takatifu; kwao kila kilichoandikwa ndani ya biblia ni sahihi. Mwelekeo huu ndio unapelekea mawazo kwamba masimulizi ya biblia yametungwa.
Biblia yote ni mafundisho ya imani na maadili; inahusu kweli za kiakili hivyo ni pia kweli za mwili.
Biblia si masimulizi ya hovyohovyo.
Biblia ni masimulizi yalio ya akili ya kina yahusuyo maisha ya mtu ya sasa na ya badae na utaratibu wa kuishi unaotakiwa. Inaeleza mwanzo wa vitu, maarifa na elimu ya vitu. Lakini pia ina vitabu vihusuyo tafiti na uzoefu binafsi wa kibinadamu kuhusu maisha.
Nashindwa jinsi ya kukujibu. Unanikumbusha presentation ya prof. Lumumba kwa Supreme Court ya Kenya kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais. Matokeo yalifutwa. Aligaragazwa licha ya systematic, verbose but smart presentation.Sijaelewa hoja yako.
Katika falsafa ya maadili tunasema matendo yanabatiza majina.
Ukiiba unaitwa mwizi.
Ukizini unaitwa mzinzi.
UKidanganya unaitwa mwongo.
Hivyo, hitimisho kwamba "Mti tunautambua kwa matunda yake," ni sahihi katika mipaka hiyo.
Mpaka hapo "mkanganyiko" uko wapi?
Pia, katika falsafa ya maadili kuna kambi ya deontoligists.
Hawa wanasema kuwa "Mtu awazavyo rohoni mwake ndivyo alivyo." kama ulivyodai.
Kuna kambi ya teleologists.
Hawa wanasema kuwa "Mtu awazavyo rohoni mwake [sivyo] alivyo."
Kwao, kilichomuhimu ni matokeo ya ulicbofikiria kufanya, ukafanya, na watu wakajua kwamba umefanya.
Watu wasipojua hakuna shida.
Hata kama umeua bado wewe sio muuaji.
Mfano:
Chukulia kuwa, umeketi katika chumba cha giza na wanawake watatu;
Halafu unajenga dhamira ya kuzini na mwanamke mmojawapo asiyemkeo;
Unapapasa na kumpata mmoja, anakulegezea, na mnakamilishana.
Deontologist kama Yesu anakuita mzinzi.
Teleologist kama nanihii anasema wewe sio mzinzi.
Baada ya haya, sasa hebu hitimisha hoja yako ili twende pamoja.
Lakini kuna ukweli mmoja nao ni huu: matendo ni muhimu kuliko maneno.
Lakini unataka mwizi atuhubirie kutokuiba
Maneno yana nafasi. Hili liko wazi.Nimependa unavyoielewa Biblia. Huko sitavinjari kwa leo. Alichosema mtu ni maneno. Mtu mwenyewe ni matendo. Kwako kuna ukweli mmoja nao ni kuwa matendo ni muhimu kuliko maneno. Je, mtu mwenyewe ni muhimu kuliko alichosema? Swali hili laweza kuwa crude! Nataraji utanielewa. Tutafika wakati tutakuwa na jambo zuri lakini siku tukijua chanzo chake tutagwaya.
Mazingira ni muhimu.Kimaadili, kauli hii yataka kujengewa uzio. Uadilifu ni tunda la vitu vitatu: dhamira, tendo na mazingira.
Wewe ama ni mwongo au una tatizo la kutoona vizuri."Kunywa coca-cola nyingi haikufanyi kuwa mchaga"...ndivo ulivyo tafsiri [emoji6][emoji6][emoji6][emoji6]
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Maneno yana nafasi. Hili liko wazi.
Hatahivyo maneno peke yake bila matendo ni kazi bure. Hayafai kitu. Hii ni kwa sababu watu hawajifunzi maneno wanajifunza matendo.
Ubongo wa mtu huchukua matendo kuliko maneno peke yake. Watu hawajengi tabia kutoka katika maneno bali katika matendo. Matendo ni undani wa mtu alivyo.
Kama mtu ni pamoja maneno na matendo ni wazi maneno pekee si muhimu kama matendo.
Kusema tu kwamba, kwa mfano, watu wanatakiwa waishi hivi hakukufanyi muhimu mpaka kunapoambatana na matendo.
Mazingira ni muhimu.
Kwa yenyewe yanastawisha au kufifisha tendo. Hayaondoi tendo lililokwisha kuwepo na hayaingizi tendo jipya ambalo halikuwepo.
Matendo hutuwezesha tufahamu uadilifu -dhamira yenyewe ya mtu ni nini.
Kama mtu anasema hivi, hiyo peke yake haitoshi. Tunahitaji kuona anavyoishi.
Kupitia maisha yake, ambayo kimsingi ndio matendo yake tutajua si tu maneno yake - anachosema, lakini dhamira yake - uadilifu wake.
Kwahiyo matendo au tendo si kile mtu anakifanya katika mazingira au hali fulani, bali matendo ni kuhusu anavyoishi mtu.
Naona kama tunaongelea vitu viwili tofauti.
Napendekeza tutofautishe praxiological analysis dhidi ya moral analysis.
Praxiological analysis iko hivi:
Ni uhambuzi ambao unaangalia maswali matatu:
Lengo la praxeological analysis ni kutuwezesha kujua kama mpango wa mtendaji umefanikiwa au hapana. Basi.
- Mtendaji alidhamiria kufukuzia lengo gani? (intention analysis)
- Mtendaji alidhamiria kutekeleza mbinu gani? (conduct analysis)
- Mtendaji ametekeleza mbinu yake lini, wapi, kwa vipi, na amezalisha matokeo aliyoyakusudia, amefeli, au amezalisha matokeo ya ziada? (circumstances analysis)
Na moral analysis iko hivi:
Ni uhambuzi ambao unaangalia maswali matatu pia:
Kutokana na maswali haya matatu kuna majibu nane yanawezekana, kama ifyatavyo:
- Lengo la mtendaji ni zuri kimaadiliau baya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani N/H)
- Mbinu yta mtendaji ni nzuri kimaadili au mbaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
- Mazingira ya kitendo ni mazuri kimaadili au mabaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
Katika matokeo haya nane yanayowezekana, kimaadili kuna njia moja pekee inayotupa msingi wa kusema mtendaji ni mwadilifu.
- NNN--Moral
- NNH--Immoral
- NHN--Immoral
- NHH--Immoral
- HNN--Immoral
- HNH--Immoral
- HHN--Immoral
- HHH--Immoral
Njia nyingine saba zinaonyesha kwamba mtendaji sio mwandilifu.
SWALI: Katika bandiko lako unafanya praxiological analysis au moral analysis?
Uje na nondo za uhakika.Here I'll be back
Nimetumia moral analysis.Bandiko lako hili pia lina mgogoro.
- Kauli hii ni kweli: "Kwa yenyewe (mazingira) yanastawisha au kufifisha tendo. Hayaondoi tendo lililokwisha kuwepo na hayaingizi tendo jipya ambalo halikuwepo."
- Kkauli hii sio kweli mara zote: "Matendo hutuwezesha tufahamu uadilifu -dhamira yenyewe ya mtu ni nini."
- Kauli hii iko out of context kabisa: "Kama mtu anasema hivi, hiyo peke yake haitoshi. Tunahitaji kuona anavyoishi."
Yaani, ni kama unadondosha maneno tu.
Tuliza akili uandike sentensi zilizoungana kimantiki ili uwawezeshe wasomaji kuona hoja yako, kuielewa na kuihakiki.
Hivyo, naomba nikurejeshe tena hapa chini ili tuweze kenda pamoja:
Ufanisi si kitu cha kufurahia kama hakileti maadili.Kusema tu kwamba, kwa mfano, watu wanatakiwa waishi hivi hakukufanyi muhimu mpaka kunapoambatana na matendo."
Lkn hiki sio kitu tunaongelea.
Pointi iliyo mezani ni uadilifu/uhalifu wa mwandishi wa Kitabu atwaye Noah Hariri
Lakini, hapa naona kama tunaongelea vitu viwili tofauti.
Napendekeza tutofautishe praxiological analysis dhidi ya moral analysis.
Praxiological analysis ni uhambuzi ambao unaangalia maswali matatu:
Lengo la praxeological analysis ni kutuwezesha kujua kama mpango wa mtendaji umefanikiwa au hapana.
- Mtendaji alidhamiria kufukuzia lengo gani? (intention analysis)
- Mtendaji alidhamiria kutekeleza mbinu gani? (conduct analysis)
- Mtendaji ametekeleza mbinu yake lini, wapi, kwa vipi, na amezalisha matokeo aliyoyakusudia, amefeli, au amezalisha matokeo ya ziada? (circumstances analysis)
Yaani, kinachoangaliwa ni effectiveness (ufanisi) peke yake.
Na tunapima ufanisi kwa kutumia vigezo vya ufanisi vilivyo katika mradi husika, na sio vinginevyo.
Hivyo, sio sawa kutumia vigezo vya maisha ya mtu au mradi A kupima ufanisi wa maisha ya mtu au mradi B.
Kwa upande mwingine, moral analysis ini uchambuzi ambao unaangalia maswali matatu lakini kwa lengo tofauti:
Kutokana na maswali haya matatu kuna majibu nane yanawezekana, kama ifyatavyo:
- Lengo la mtendaji ni zuri kimaadili au baya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani N/H)
- Mbinu yta mtendaji ni nzuri kimaadili au mbaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
- Mazingira ya kitendo ni mazuri kimaadili au mabaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
Katika matokeo haya nane yanayowezekana, kimaadili kuna njia moja pekee inayotupa msingi wa kusema mtendaji ni mwadilifu.
- Ndiyo-Ndiyo-Ndiyo--Mtendaji ni mwadilifu
- Ndiyo-Ndiyo-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
- Ndiyo-Hapana-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
- Ndiyo-Hapana-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
- Hapana-Ndiyo-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
- Hapana-Ndiyo-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
- Hapana-Hapana-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
- Hapana-Hapana-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
Njia nyingine saba zinaonyesha kwamba mtendaji sio mwandilifu.
Yaani, "hapana" moja tu inatosha kutia doa wasifu wake wa kimaadili.
Lengo la moral analysis ni kutuwezesha kujua kama mtendaji ni mtu mwadilifu au hapana.
Yaani, kinachoangaliwa ni moral status, basi.
KWA HIYO SWALI: Katika bandiko lako unafanya praxiological analysis au moral analysis?
Nimekuelewa.Nimetumia moral analysis.
Sifahamu kwako matendo au tendo ni nini.
Sawa ambavyo ni vigumu kufafanua uadilifu bila kuangalia dhamira ndivyo pia haiwezekani kutenganisha maisha kutoka katika matendo.
Katika mukutadha wa uadilifu, matendo au tendo ni jinsi anavyoishi mtu.
Nafafanua.
Tendo au matendo ya mara moja hayawezi peke yake kutumika kufanya moral analysis.
Kwa sababu moral analysis inaangalia maisha yote ya mtu. Unatendaje katika mambo msingi ya maisha.
Dhamira ya mtu katika jambo lolote haifafanuliwi na tendo mara moja au mazingira fulani, nafasi au mamlaka bali maisha anayoishi.
Kupima dhamira ambayo kimsingi huwezesha kufahamu uadilifu wa mtu tuangalia maisha anayoishi yeye na maisha wanaoishi jirani zake.
Tendo la kuiba kwa lenyewe ni kosa kimaadili.Lakini nina swali dogo:
Kitendo cha kuiba tunakifanyiaje moral analysis?
Tendo la kuiba kwa lenyewe ni kosa kimaadili.
Huwezi kufanya tendo baya ili humo litoke tendo jema.
Mbinu ovu haifanyi kilichopatikana kiwe chema.
Dhamira njema haifanyi tendo baya.
Mimi nionavyo ni kuwa hakuna tendo au jambo ovu ambalo likifanyika athari zake ni nafuu.Asante kwa ufafanuzi.
Mwaka 1968 wakati Kanisa Katoliki linajadili matumizi ya kingamimba, watetezi wa kingamimba walijenga hoja kuwa
1. Some of the marital sexbacts are evil, when contraception is used
2. Some are not in the absence of contraception, coercion, deception, etc
3. So, a morality of marital sex life should be judged from the net sum of individual sex acts.
Hoja hii ilikataliwa na Papa Paul VI kwa sababu kwamba ina msingi wake ktk proportionalism-- determining moral status of an actor by balancing insividual good and evil acts.
Yaani kama mtu amefanya vitendo kumi vya kutoa taarifa. Halafu, kati yake alidanganya mara nne na kusema ukweli mara sita anakuwa ni mwadilifu.
Unayo maoni gani juu ya moral methodology hii ya proportionalism?
Mimi nionavyo ni kuwa hakuna tendo au jambo ovu ambalo likifanyika athari zake ni nafuu.
Sio sahihi kufikiri kuwa, kwa mfano, athari za tendo uovu la kutoa mimba na athari za tendo ovu la kutumia vizibiti mimba; eti kwamba mojawapo kati ya matendo hayo athari zake ni nafuu. Kwahiyo ni uadilifu, hapana.
Uamuzi wa Papa ulikuwa sahihi na hii ni asili yenyewe.
Tendo au jambo ovu ni ovu tu. Sio suala la nini tendo hilo au jambo hilo linazalishwa.
Najua unazungumzia 'Formal' education,Swali langu je Informal education haina 'mantiki'? Kuna watu wako na uzoefu wa kutosha katika maisha na kama msemo pendwa 'experience is a best teacher',Nakubaliana nawe.
Hata viongozi wa dini zetu pendwa za Ukristo na Usilam wanapitia barabara hiyo.
Tanzania ina watu wenye elimu ya kidato cha 4 au zaidi walio chini ya 10%, per UNESCO's data.
Kwa hiyo, watu 90% wanaongozwa na hoja zinazooanzia kwenye hisia badala ya hoja zinazooanzia kwenye mantiki.
Tupanue education attainment level ya nchi angalau kufikia F4 education attainment level ya 51%, na mengine yatafuata.