Masomo 21 Kwa Ajili ya karne ya 21: Ukweli Kinyonga, Kuna Ukweli Bandia Unaodumu Milele

Nimependa unavyoielewa Biblia. Huko sitavinjari kwa leo. Alichosema mtu ni maneno. Mtu mwenyewe ni matendo. Kwako kuna ukweli mmoja nao ni kuwa matendo ni muhimu kuliko maneno. Je, mtu mwenyewe ni muhimu kuliko alichosema? Swali hili laweza kuwa crude! Nataraji utanielewa. Tutafika wakati tutakuwa na jambo zuri lakini siku tukijua chanzo chake tutagwaya.
 
Nashindwa jinsi ya kukujibu. Unanikumbusha presentation ya prof. Lumumba kwa Supreme Court ya Kenya kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais. Matokeo yalifutwa. Aligaragazwa licha ya systematic, verbose but smart presentation.
Unanipa swali na ushauri ambao, pengine bila kujua, wewe mwenyewe umejijibu. Umeanza kwa kutambua mti kwa matunda yake. Kwako pia, mchungwa haukuzaa komamanga. Lakini unataka mwizi atuhubirie kutokuiba. Tuangalie hoja na si mleta hoja. Labda kama ilivyo kwa saa mbovu kuonyesha majira sahihi. Si imesoma? Lakini ni nadra sana. Uanza wazo akilini litakalozaa matendo/matokeo. Wazo linatokana na imani ya mhusika.
 
Maneno yana nafasi. Hili liko wazi.

Hatahivyo maneno peke yake bila matendo ni kazi bure. Hayafai kitu. Hii ni kwa sababu watu hawajifunzi maneno wanajifunza matendo.

Ubongo wa mtu uchukua matendo kuliko maneno peke yake. Watu hawajengi tabia kutoka katika maneno bali katika matendo. Matendo ni undani wa mtu alivyo.

Kama mtu ni pamoja maneno na matendo ni wazi maneno pekee si muhimu kama matendo.

Kusema tu kwamba, kwa mfano, watu wanatakiwa waishi hivi hakukufanyi muhimu mpaka kunapoambatana na matendo.
 
Kimaadili, kauli hii yataka kujengewa uzio. Uadilifu ni tunda la vitu vitatu: dhamira, tendo na mazingira.
Mazingira ni muhimu.

Kwa yenyewe yanastawisha au kufifisha tendo. Hayaondoi tendo lililokwisha kuwepo na hayaingizi tendo jipya ambalo halikuwepo.

Matendo hutuwezesha tufahamu uadilifu -dhamira yenyewe ya mtu ni nini.

Kama mtu anasema hivi, hiyo peke yake haitoshi. Tunahitaji kuona anavyoishi.

Kupitia maisha yake, ambayo kimsingi ndio matendo yake tutajua si tu maneno yake - anachosema, lakini dhamira yake - uadilifu wake.

Kwahiyo matendo au tendo si kile mtu anakifanya katika mazingira au hali fulani, bali matendo ni kuhusu anavyoishi mtu.
 

Umeandika:

"Kusema tu kwamba, kwa mfano, watu wanatakiwa waishi hivi hakukufanyi muhimu mpaka kunapoambatana na matendo."

Lkn hiki sio kitu tunaongelea.

Pointi iliyo mezani ni uadilifu/uhalifu wa mwandishi wa Kitabu atwaye Noah Hariri

Lakini, hapa naona kama tunaongelea vitu viwili tofauti.

Napendekeza tutofautishe praxiological analysis dhidi ya moral analysis.

Praxiological analysis ni uhambuzi ambao unaangalia maswali matatu:
  1. Mtendaji alidhamiria kufukuzia lengo gani? (intention analysis)
  2. Mtendaji alidhamiria kutekeleza mbinu gani? (conduct analysis)
  3. Mtendaji ametekeleza mbinu yake lini, wapi, kwa vipi, na amezalisha matokeo aliyoyakusudia, amefeli, au amezalisha matokeo ya ziada? (circumstances analysis)
Lengo la praxeological analysis ni kutuwezesha kujua kama mpango wa mtendaji umefanikiwa au hapana.

Yaani, kinachoangaliwa ni effectiveness (ufanisi) peke yake.

Na tunapima ufanisi kwa kutumia vigezo vya ufanisi vilivyo katika mradi husika, na sio vinginevyo.

Hivyo, sio sawa kutumia vigezo vya maisha ya mtu au mradi A kupima ufanisi wa maisha ya mtu au mradi B.

Kwa upande mwingine, moral analysis ini uchambuzi ambao unaangalia maswali matatu lakini kwa lengo tofauti:
  1. Lengo la mtendaji ni zuri kimaadili au baya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani N/H)
  2. Mbinu yta mtendaji ni nzuri kimaadili au mbaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
  3. Mazingira ya kitendo ni mazuri kimaadili au mabaya kimaadili? (Ndiyo/Hapana, yaani yaani N/H)
Kutokana na maswali haya matatu kuna majibu nane yanawezekana, kama ifyatavyo:

  1. Ndiyo-Ndiyo-Ndiyo--Mtendaji ni mwadilifu
  2. Ndiyo-Ndiyo-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
  3. Ndiyo-Hapana-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
  4. Ndiyo-Hapana-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
  5. Hapana-Ndiyo-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
  6. Hapana-Ndiyo-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
  7. Hapana-Hapana-Ndiyo--Mtendaji sio Mwadilifu
  8. Hapana-Hapana-Hapana--Mtendaji sio Mwadilifu
Katika matokeo haya nane yanayowezekana, kimaadili kuna njia moja pekee inayotupa msingi wa kusema mtendaji ni mwadilifu.

Njia nyingine saba zinaonyesha kwamba mtendaji sio mwandilifu.

Yaani, "hapana" moja tu inatosha kutia doa wasifu wake wa kimaadili.

Lengo la moral analysis ni kutuwezesha kujua kama mtendaji ni mtu mwadilifu au hapana.

Yaani, kinachoangaliwa ni moral status, basi.

KWA HIYO SWALI: Katika bandiko lako unafanya praxiological analysis au moral analysis?
 

Bandiko lako hili pia lina mgogoro.

  • Kauli hii ni kweli: "Kwa yenyewe (mazingira) yanastawisha au kufifisha tendo. Hayaondoi tendo lililokwisha kuwepo na hayaingizi tendo jipya ambalo halikuwepo."
  • Kkauli hii sio kweli mara zote: "Matendo hutuwezesha tufahamu uadilifu -dhamira yenyewe ya mtu ni nini."
  • Kauli hii iko out of context kabisa: "Kama mtu anasema hivi, hiyo peke yake haitoshi. Tunahitaji kuona anavyoishi."

Yaani, ni kama unadondosha maneno tu.

Tuliza akili uandike sentensi zilizoungana kimantiki ili uwawezeshe wasomaji kuona hoja yako, kuielewa na kuihakiki.

Hivyo, naomba nikurejeshe tena hapa chini ili tuweze kenda pamoja:

 
Nimetumia moral analysis.

Sifahamu kwako matendo au tendo ni nini.

Sawa ambavyo ni vigumu kufafanua uadilifu bila kuangalia dhamira ndivyo pia haiwezekani kutenganisha maisha kutoka katika matendo.

Katika mukutadha wa uadilifu, matendo au tendo ni jinsi anavyoishi mtu.

Nafafanua.

Tendo au matendo ya mara moja hayawezi peke yake kutumika kufanya moral analysis.

Kwa sababu moral analysis inaangalia maisha yote ya mtu. Unatendaje katika mambo msingi ya maisha.

Dhamira ya mtu katika jambo lolote haifafanuliwi na tendo mara moja au mazingira fulani, nafasi au mamlaka bali maisha anayoishi.

Kupima dhamira ambayo kimsingi huwezesha kufahamu uadilifu wa mtu tuangalia maisha anayoishi yeye na maisha wanaoishi jirani zake.
 
Ufanisi si kitu cha kufurahia kama hakileti maadili.

Kama tutangalia ufanisi peke yake maana yake hatujali nini kinazalishwa ila hicho kilichozalishwa.

Anayezingatia ufanis peke yake maana yake ameshindwa kujifunza katika maumbile.

Maisha ya mtu, jinsi anavyoishi ni muhimu zaidi kuliko maneno yake anayoyasema au anayoandika.

Ukweli huu tunaupata kwa Yesu mwenyewe, maisha yake ambayo ndio matendo yake yanaweka umuhimu zaidi na kuyapa maana maneno yake.
 
Nimekuelewa.

Lakini nina swali dogo:

Kitendo cha kuiba tunakifanyiaje moral analysis?
 
Tendo la kuiba kwa lenyewe ni kosa kimaadili.

Huwezi kufanya tendo baya ili humo litoke tendo jema.

Mbinu ovu haifanyi kilichopatikana kiwe chema.

Dhamira njema haifanyi tendo baya.

Asante kwa ufafanuzi.

Miaka ya 1960 wakati Kanisa Katoliki linajadili uadilifu wa matumizi ya kingamimba, watetezi wa kingamimba walijenga hoja kuu ifuatayo:
  1. Some of the marital sex acts performed by married personsare morally good, by reasons associated with the absence of contraception, coercion, deception, pedication, fellatiation, and masturbation.
  2. Some sex acts performed by married persons are morally evil by reasons associated with contraception, coercion, deception, pedication, fellatiation, and masturbation.
  3. So, given that married life is a totality, the morality of sexual life married persons should be judged based on the net sum of their individual sex acts.
Hoja hii ilikataliwa na Papa Paul VI kwa sababu kwamba kila tendo la binadamu linao uadilifu na uharamu wake ambao hauwezi kubadilishwa na uadilifu au uharamu wa tendo jingine. Yaani, alikataa hoja ya kutafuta uwiano wa asilimia ya matendo mema na asilimia ya matendo mabaya ndani ya kipindi fulan kama msingi wa kimaadili. Hii ni proportionalism-- determining moral status of an actor by balancing individual good acts and individual evil acts . Kwa mfano:
  1. Kama mtu amefanya tendo la ngono mara 20 kwa mwezi, na kati yake 9 ni matendo ya kumlazimisha mwenza wake, basi, kwa wastani, mtu huyo ni mwadilifu, kwa sababu asilimia ya matendo halali ya ngono ni kubwa kuliko asilimia ya matendo haramu.
  2. Kama mtu amefanya vitendo kumi vya kutoa taarifa, halafu, kati yake alidanganya mara nne na kusema ukweli mara sita anakuwa ni mwadilifu, kwa kuwa asilimia ya kauli za kweli ni kubwa kuliko asilimia ya kauli za uwongo.
  3. Na kama mfanya biashara amekwepa kodi kwa miezi mitano na kulipa kodi kwa miezi saba anakuwa ni mwadilifu kwa kuwa asilimia ya miezi aliyolipa kodi ni kubwa kuliko asilimia ya miezi aliyokwepa kodi.
Hii inaitwa methodolojai ya kutafuta uwiano wa kimaadili kwa kuwa inaruhusu uwianishaji wa mema na mabaya (proportionalism). Unayo maoni gani juu ya moral methodology hii ya proportionalism, mbinu ya kupima uadilifu wa mtu kwa kutafuta wastani wa matendo yake mema na matendo yake mabaya?
 
Mimi nionavyo ni kuwa hakuna tendo au jambo ovu ambalo likifanyika athari zake ni nafuu.

Sio sahihi kufikiri kuwa, kwa mfano, athari za tendo uovu la kutoa mimba na athari za tendo ovu la kutumia vizibiti mimba; eti kwamba mojawapo kati ya matendo hayo athari zake ni nafuu. Kwahiyo ni uadilifu, hapana.

Uamuzi wa Papa ulikuwa sahihi na hii ni asili yenyewe.

Tendo au jambo ovu ni ovu tu. Sio suala la nini tendo hilo au jambo hilo linazalishwa.
 

Sawa. Lkn mbona maelezo yako ya awali kuhusu uadilifu wa mtu yanaegemea kwenye proportionalism?

Umesema kuwa haiwezekani kupima uadilifu wa mtu kwa kuangalia tendo moja moja, bali maisha yake over a period of time.

Ndio maana nikakuomba ufanye moral analysis ya tendo moja la kuiba ili nione approach yako.

Katika waraka wa Humanae Vitae papa alitumia maneno "principle of totality". Lkn ni kitu kile kile.

Kwa ufupi nimekuelewa.

Mimi naikataa moral proportionalism, principle of totality, and the like.

Kanuni hii inahalalisha kila uovu unaoweza kufikirika hapa duniani.

Mfano, kwa mujibu wa principle of totality, ni afadhali mtu mmoja afe ili kuikoa kikundi cha watu kumi.

Madikteta wote wa dunia walitumia mbinu huu.
 
Najua unazungumzia 'Formal' education,Swali langu je Informal education haina 'mantiki'? Kuna watu wako na uzoefu wa kutosha katika maisha na kama msemo pendwa 'experience is a best teacher',
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…