mi naona Hajachochea kaelimisha, pengine waliomkamata hawajaelewa vizuri io picha ni vizuri wakarudi fom 3 Wakasome vizuri fasihi
Nafikiri kwenye hio katuni kipanya anataka kuieleza jamii kuwa serikali inategemea kodi kuendesha shughuli zake za kila siku, na hio ni kweli serikali zote duniani hutegemea mapato ya kodi kuendesha shughuli zote za kiserikali kama kulipa mishahara, kulipa miradi ya maendeleleo n.k.
Serikali nyingine kama za uarabuni wana bahati, wanaweza kuchimba mafuta wakaendesha nchi lakini bado hitaji la kukusanya kodi liko pale pale ko nimemwelewa mchoraji kuwa kodi ndio silaha pekee inayotegemewa kuendesha serikali.
Hivo basi ni vizuri vyombo vyetu vya dola vikaelewa fasihi kwa mapana na marefu yake