Masoud Kipanya adaiwa kukamatwa kwa kuchora katuni ya kichochezi. Yeye aibuka, adai aliyetoa taarifa 'AMESAIDIA'

Masoud Kipanya adaiwa kukamatwa kwa kuchora katuni ya kichochezi. Yeye aibuka, adai aliyetoa taarifa 'AMESAIDIA'

Kukosoa serikali ni jambo la kikatiba na huwezi kuiondoa!! Sema nyinyi mngependa watu wamuabudu huyu mtu. Mnasahau hata hesabu ya kura 2015 mlitengeneza kupata percentage. Serikali kukosolewa ni afya
Hakuna mtu ambaye amekataza Serikali isikosolewe, lakini kila jambo lina mipaka yake. Uandishi wa habari una mipaka yake na kuna namna inayokubalika ya kuwasilisha habari husika. Na ndiyo maana sheria zikawekwa, ili yeyote atakayevuka mipaka husika basi sheria wacha ichukue mkondo wake.
Kila nchi duniani iliyostaarabika inazo sheria za kushughulikia maswala mbali mbali. Na sheria hizi haziwezi kufanana. Unaweza ukafanya kitu Marekani ikawa ni sawa tu, lakini kitu hicho hicho ukikifanya Uturuki unakamatwa na kushtakiwa. Ndivyo ilivyo ndugu. Kila nchi ina taratibu zake ilizojiwekea.
 
cea0212850d744cd158154623946b1d9.jpg
[emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41]
Duh Hii ndio Imemponza?
 
Mahakamani wakiuluzwa ni wapi ameitaja serikali ya Tanzania watajibu nini maana serikali ziko nyingi katika hii dunia na zote zinatoza kodi.

Hamna kesi hapo bali lengo ni kumtisha tu.
Watajibu wamejijua ni wao tu kwa maana nchii hii viumbe hao wamejizoesha kuwa na kiherere sana na kiki sasa mpaka na panya wanaongeaongea.
 
Ni kweli aisee?Hebu tuhakikishieni...

Hii ni vituko aisee

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Aibu sana
 
Dah kumuenzi inabidi katuni zake zisambazwe kila eneo.....huyu jamaa no zaidi ya James gayo. ....hope yupo ok
 
Hakuna mtu ambaye amekataza Serikali isikosolewe, lakini kila jambo lina mipaka yake. Uandishi wa habari una mipaka yake na kuna namna inayokubalika ya kuwasilisha habari husika. Na ndiyo maana sheria zikawekwa, ili yeyote atakayevuka mipaka husika basi sheria wacha ichukue mkondo wake.
Kila nchi duniani iliyostaarabika inazo sheria za kushughulikia maswala mbali mbali. Na sheria hizi haziwezi kufanana. Unaweza ukafanya kitu Marekani ikawa ni sawa tu, lakini kitu hicho hicho ukikifanya Uturuki unakamatwa na kushtakiwa. Ndivyo ilivyo ndugu. Kila nchi ina taratibu zake ilizojiwekea.
Umemàliza? Maana povu limekutoka sana, halafu unafananisha USA na Uturuki? Ufahamu wako naona umepungua sàna. Nchi zote zinazominya demokrasia ndio zenye sheria kandamizi, mfn: Russia, Uturuki, Irani, Tanzania, Rwànda, Uganda na zingine nyingi tu. Làkini nchi zenye uhuru wa demokrasia mfn: USA, UK, Germàny, Kenya na NK hutaona upumbavu kama huo.
 
Back
Top Bottom