Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa mujibu wa Wakili wa Masoud Kipanya, amesema Mtangazaji huto maarufu kwasasa anapata shida kujitokeza mbele ya watu kutokana na tuhuma za kujihusisha biashara haramu zilizotolewa na Mwijaku

Hayo yamebainishawa na Wakili wa Mtangazaji Masoud Kipanya, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates ambapo amedai mmteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya naye kazi.

Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au alipe Tsh 5 Bilioni.



photo_2024-06-15_18-39-16 (2).jpg

Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba

Mchora katuni maarufu, Ally Masoud Nyomwa “Masoud Kipanya”, anakusudia kumshtaki Mahakamani na kumdai fidia ya Tsh. Bilioni 5, Burton Mwemba Mwijaku kwa madai kumkashifu na kuandika maudhui ya uongo dhidi yake katika ukurasa wake wa Mtandaoni wa Facebook ambayo pia yanadaiwa kusambaa kwenye kurasa nyingine.

Ikielezwa kuwa hali hiyo imesababisha kumshushia heshima na kupelekea baadhi ya taasisi kusita kufanya naye kazi mbalimbali.

Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ni Wakili wa Kipanya ameyasema hayo Juni 14, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Wakili huyo akizungumzia suala hilo mbele ya Vyombo vya Habari anasema Mwijaku alitoa maneno ya uongo bila ushahidi, kwamba Kipanya anabiashara haramu na ambayo imechangia kuharibu vijana wengi.

Madai mengine ambayo Wakili anadai yalitolewa na Mwijaku ni kwamba Kipanya amezoea kuwazodoa viongozi wa Nchi na marais kwa kuwadhalilisha pamoja na madai Kipanya amekuwa akihongwa kuichafua Serikali na viongozi wake.

Wakili huyo amesema Kipanya kabla ya kuja mbele ya Vyombo vya Habari na Umma alimpa siku tatu Mwijaku kuomba radhi kwa uzito uleule aliotumia kumchafua sambamba lakini siku tatu zilipita bila kufanya alivyoelekezwa.

Anasema barua hiyo iliyoandikwa Juni 7, 2024 na kupokelewa siku tatu tokea siku hiyo, ilimwelekeza Mwijaku kujitafakari na kuomba radhi kwa maandishi kupitia mitandao yote aliyotumia.

Aidha, amedai licha ya uwepo wa taarifa inayodaiwa kuwa ni 'Press Release' iliyotolewa na Mwijaku amesema Mteja wao msimamo wake kwa sasa ni kwamba anaona kwamba njia pekee ya kutumika kumrejeshea heshima yake ni Mahakama.

Wakili huyo amesema madai ambayo yametolewa na Mwijaku dhidi ya Kipanya hayana ukweli wowote na kuwa yameendelea kumuathiri mteja wao ambaye amekuwa akifanya majukumu yake yanayogusa jamii kwa uchanya.

Amesema kwa kuwa madai hayo yanagusa mamlaka nyingine, ameeleza matarajio yao kwa Vyombo vya dola na taasisi nyingine zitakuwa zinachukua hatua, lakini amedai kwa upande wao pia wapo tayari kutoa ushirikiano kulingana na taratibu.

Amesisitiza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ambayo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa, inatoa uhuru wa kujieleza lakini pia uhuru huo una wajibu.

Pia Soma:

- Mwijaku amwandikia Waraka Mzito Masoud Kipanya, adai anafanya biashara haramu

- Mwijaku amuomba msamaha Masoud Kipanya baada ya kumtuhumu kuwa “anafanya biashara haramu” na kutukana Viongozi akiwemo Rais

- Mwijaku aandikiwa hati ya Madai ya Tsh. Milioni 300 kwa kumdhalilisha Maua Sama
 
Back
Top Bottom