Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Funzo ni mtuhumiwa kulipa faini akikutwa na hatia au kifungo akishindwa zaidi ya hapo hii michezo ya kuigiza itaendelea kuwepo
Hivi ukiangalia dhihaka, matusi wanayotukana hao watu halafu wajanja mwisho wanamalizia watoto wa mama, namuunga mkono mama , mama mitano tena unawaangalia unasema hawa watoto wajinga sana
 
Kuna vijana wa hovyo sana tumefanya makosa sana kuwapa nafasi ya kuwa sikiliza kwenye jamii yetu kwa siku za karibuni, matokeo yake ndiyo hayo. Wameenda mbali na kujifananinisha na mdudu chawa. Chawa/machawa sasa wamekua wanaropoka ropoka tu.Bado na yule mwingine sijuwi alipata vipi udiwani enzi hizo.
 
Ningemshangaa Sana Masoud endapo angepokea msamaha uchwara wa Mwijaku ilhali tiyari brand yake imeshachafuliwa, Mimi binafsi nilishaanza kuamini alichokisema Mwijaku Japo sina uthibitisho.


Mwijaku ili aweze kuchunga kinywa chake wakati mwingine basi anatakiwa kukutana na faini itakayomuacha Fukara , vinginevyo hawezi kukoma huyu
 
Kipanya hana nywele lakini katumia akili sana, naona amechagua kumdhalilisha Mwijaku kisomi zaidi ,
Kwa maana si anatamba ana mali za mabilioni haya tema bungo bilioni tano hizo ambazo kwa ukweli kabisa bwana yule hawezi kua nayo mwisho atatia tia huruma na kutembea na magoti yaishe
 
Watauza lile ghorofa ile Noah na Alphard akajifunze.

Kwa jinsi sheria zilivyo Ghorofa haliwezi kuuzwa na mahakama sababu. Ni matrimonial property. Mwijaku sio lake peke yake. Na Mke wa mwijaku hausiki kwenye hiyo kesi ya madai.

Mahakama itakwama kukamata ghorofa.

Kesi za madai ni ngumu sana kwenye kukamata mali za wanandoa. Kesi za madai ni nyepesi sana kama unaidai kampuni. Maana kampuni haiingiliwi na watu. Hivyo mali za kampuni unazikamata tu na kuziuza.

Pia kesi za madai zina ujinga wa kulipa kidogo kidogo. Hata elfu 10 kwa mwezi ruksa
 
Back
Top Bottom