Unakuwa tu na bonge la compound. Watoto wanacheza pamoja, wanajifunza pamoja, wanafurahi pamoja. Na nyumba zinakuwa za kutosha, za kisasa, magari ya kufanyia kazi, kupeleka watoto shule pia yawepo ya kutosha na ya uhakika, na wives pia wawe wanafanya kazi kwa biashara, na watoto wanajifunza kazi pamoja, biashara pamoja, wanapata burudani kama movies pamoja, mnasali pamoja, nk. Naona imekaa vizuri sana.. cha muhimu unakuwa tu mkuu wa Boma mwenye hekima ya uongozi na heshima iwepo pote manake kila mtu amheshimu mwingine pamoja na wives na watoto waheshimiane na wapendane.