Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya KAYPEE MOTORS, ambae pia ni Mtangazaji kutoka kituo cha Clouds Media Group, Ally Masoud Nyomwa maarufu kama Masoud Kipanya, ametunukiwa shahada ya heshima katika kutambua mchango wake kwa Jamii, ubunifu na ustahimilivu, ambayo inatambulika kama Vanguard Honorary Degree for Creativity, Resilience and Social Impact.
View attachment 3171410
Ametunukiwa shahada hiyo wakati wa mahafali ya tano ya Chuo cha usimamizi wa miradi, ufuatiliaji na uhakiki wa ubora Tanzania TIPM (Tanzania Institute of Project Management), Jijini Dar es salaam.
View attachment 3171412
Hongera sana Masoud Kipanya.