Masoud Kipanya atunukiwa Shahada ya Heshima (Vanguard Honorary Degree for Creativity)

Masoud Kipanya atunukiwa Shahada ya Heshima (Vanguard Honorary Degree for Creativity)

Shahada ya uvumilivu na ustahimilivu...navumilia mengi sana ipo siku na mimi. Hongera sana kp huwa unapata shida pale power breakfast watangazaji wenzako kukuelewa unachomaanisha.
 
Hizi shahada za heshima zitolewe na vyuo vikuu vinavyotambulika kimataifa itakuwa heshima zaidi. Isiwe kila chuo tu kikiamua kumpa mtu hadhi hiyo kinampa. Vyuo vingine ni vituko tu vinashusha hadhi shahada hizo
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya KAYPEE MOTORS, ambae pia ni Mtangazaji kutoka kituo cha Clouds Media Group, Ally Masoud Nyomwa maarufu kama Masoud Kipanya, ametunukiwa shahada ya heshima katika kutambua mchango wake kwa Jamii, ubunifu na ustahimilivu, ambayo inatambulika kama Vanguard Honorary Degree for Creativity, Resilience and Social Impact.

View attachment 3171410

Ametunukiwa shahada hiyo wakati wa mahafali ya tano ya Chuo cha usimamizi wa miradi, ufuatiliaji na uhakiki wa ubora Tanzania TIPM (Tanzania Institute of Project Management), Jijini Dar es salaam.
View attachment 3171412

Hongera sana Masoud Kipanya.
Big up brother Kipanya you deserve it [emoji122]
 
Huwa haziitwi PhD (Doctor of Philosophy). Ni degree za heshima "kutambua mchango" wa mhusika. Neno "philosophy" halimo kwenye hizo titles! Rather, utasikia Doctor of Letters (Honoris Causa) and similar titles; not a PhD.
Na mimi huwa wananiudhi sana kuilinganisha PhD na mambo ya ujinga.
 
Back
Top Bottom