DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mahojiano yao kwa maneno yakuwa
Mwandishi wa Bongo FM: Sawa sawa. Pengine kwenye eneo ambalo pengine ukilitazama unaona ni hapa nikitazama, huu ni mwiba ambao unachangia labda vijana wengi wa bunifu, wana mawazo ambayo wanaweza wakaimplement wakafanya kazi linakwamisha yaani ni eneo lipi mahususi ukiona kabisa jamani hili tulikate tulitoe linachelewesha watu kufikia ndoto zao kwenye ubunifu?
Kipanya: Walio kuwa kwenye nafasi za maamuzi. Watu ambao wako kwenye vyombo mbalimbali. Wakurugenzi wa idara mbalimbali. Unapozungumzia kwa sababu unajua sisi mlango geti la mwisho kabisa kufika kwa wananchi ni kwenye halmashauri kwa mfano. Kwenye halmashauri pale kuna idara zote ambazo zinamhusu mtu. Unajua kwa kwa vijana unajua unapozungumzia masuala ya maendeleo ya jamii, kila kitu kipo.
Lakini sasa, sio watu wote sio watumishi wote kweli wamewaliwa kufanya mambo kwa ajili ya watu wengine. Watumishi walio wengi wanachoangalia ni mshahara ambao wanalipwa, amemaliza. Ah sidhani kama wana kitu kinachoitwa KPI kwamba, "Bana wewe unapangiwa ndani ya mwezi ufanye moja, mbili, tatu na tuone kinachokamilika na kinachosimamiwa." Kwa hiyo kusema ukweli, wanaotukwamisha kwa kiasi kikubwa sana ni watumishi...
Nitakupa mfano, kwenye kila halmashauri kuna asilimia 10 inayotolewa kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Ah na asilimia 10 inayokwambia ni asilimia 10 ya pato la ile halmashauri. Kuna halmashauri hapa zinapokea mabilioni ya fedha kwa mwaka, kwa hiyo ukiweka 10 percent yake bado ni hela nyingi sana.
Lakini sasa bado unakuja unakuta vikundi kuna vikundi hewa vimetengenezwa, kuna watu wanapewa hela hawazirudishi... Hivi wewe kweli mimi nikupe nikupe wewe hela na nishindwe vipi kukufuatilia wewe mpaka nihakikishe hiyo pesa uliyokopesha unairudisha ili mwingine tena achukue? Ni kwa sababu ya ndio hiyo aidha vitu vinatengenezwa vinakuwa ni hewa au watu hawafanyi kazi zao, maanake wewe umempa mtu hela alafu humfuatilii au umesajili kikundi umekipa kikundi hela alafu hukijui, kwa hiyo kikipotea hujui. Kwa hiyo kweli ni kwamba sehemu kuna sehemu sio wote kuna sehemu kubwa sana ya watumishi ambao wana iangusha Tanzania.
Unaonaje hoja yake