Masoud Masoud, Manju wa muziki ni nani?

Huyu anajuwa miziki

Nilimsikiliza siku moja anakuambia

Kwanini wasanii wa tz hawawezi kushiriki tuzo za grammies

Ova
 
Huyu mwamba ametisha sana akuna wa kumkaribia hata chembe.
Kuna bwana mmoja anaitwa Miguel Suleiman. Alikuwa akiandika makala za muziki katika gazeti la The Guardian, Nipashe na mengine ya IPP.

Pia alikuwa akialikwa Radio One miaka ya nyuma kuchambua Muziki.

Huyu hata Masoud Masoud anamjua. Ni gwiji wa muziki ambaye ameufanyia tafiti katika sehemu kadhaa duniani.

Kwa sasa sijui yupo wapi. Ila kwangu Huyu ndiye Hana mpinzani. Wengi nadhani hawamjui.

Aliwahi kufundisha Somo la lugha ya kifaransa katika shule ya sekondari Forodhani miaka ya nyuma.

Shule ya Forodhani wanaijua wahenga wenzangu tu.
 
Kipindi chake kipo muda Gani?
 
Machinga uenda na upepo kuwahi pesa.
Soko ndilo uamua aina ya muziki
 
heshima kwake🙏.
huyo ana kipaji cha juu,ingawa sio maarufu lakini mimi huwa naamini maneno ya wahenga.
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=lBz6v8evdQM
 
hawa tbc siwapati kabisa online sijajua kama unatumia njia gani mkuu
 
.
Mshawishini awemo humu,,tumuhoji,,,tutapata meeengi ambayo yatahifadhika humu,SI unajua kila nafsi inakaburi lake.
Angalia post ya juu, au nenda YouTube. Alishaelezea mengi kuhusu maisha yake. Huyu ni raslimali ya Taifa letu. Siyo hawa washenzi kina Kitenge, wanaongeoa kama cherehani lakini hakuna cha maana.
 
Huyu Bwana kama angepata wadhamini au Serikali ikamsaidia kutekeleza Mawazo yake hasa tungeweza kuwa na pakuanzia, Wizara ya Utamaduni wangeona ni wapi huyu bwana anaweza kufiti na kuanzisha vionjo vya Music wa Tanzania
Ndugu yangu hii nchi viongozi wengi wanapata nafasi zao kwa kubebwa au awe Chawa,kwa Aina hiyo hatuwezi Pata kiongozi mwenye maono ya mbali kabisa kwa nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…