Mastaa wenye mvuto zaidi kwenye Jamii

Mastaa wenye mvuto zaidi kwenye Jamii

Bila shaka hawa ni wasanii wanaotokea sana kwenye Magazeti ya Global Publisher wenye viskendo skendo
 
warumi hii ni orodha ya masuper star au Bongo movie?

Diamond na jide wapo bongo movies?? Wengi niliowataja wapo bongo movies , kwan hawafai kaka??
 
Last edited by a moderator:
Diamond na jide wapo bongo movies?? Wengi niliowataja wapo bongo movies , kwan hawafai kaka??

Kukubali kukosea ni uungwana Bongo hakuna superstar wa kumzidi Okwi, Samatta na Ngasa, hao uliorodhesha hakuna mwenye uwezo wa kuujaza uwanja wa Taifa.

sina nia ya kukukatisha tamaa ila next time wapange kwa category.
 
Me hapo namjua jay dee na jb,hao wengine hata siwajui.
 
I think ther'z a great need of research....ingawa orodha ina uhalisia kwa asilia kubwa 2
 
Kukubali kukosea ni uungwana Bongo hakuna superstar wa kumzidi Okwi, Samatta na Ngasa, hao uliorodhesha hakuna mwenye uwezo wa kuujaza uwanja wa Taifa.

sina nia ya kukukatisha tamaa ila next time wapange kwa category.

Mmh, sijakuelewa , ila kumbuka hawa ni mastaa wa bongo nazungumzia sasa sielewi hao wakina okwi wamekujaje.

Ni wasanii gani hapa Om ambao unadhan wana mvuto kuliko hawa niliowataja?? Hili ndo la muhimu
 
Mmh, sijakuelewa , ila kumbuka hawa ni mastaa wa bongo nazungumzia sasa sielewi hao wakina okwi wamekujaje.

Ni wasanii gani hapa Om ambao unadhan wana mvuto kuliko hawa niliowataja?? Hili ndo la muhimu
sasa nimekuelewa ni wasanii.
 

Attachments

  • 1398012442393.jpg
    1398012442393.jpg
    42.7 KB · Views: 219
Ukiachilia mbali wingi wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia mbali mbali apa bongo, sio wote wanaobahatika kukubalika na kupokelewa vizuri na Jamii/mashabiki. Hawa ndio wasanii wenye mvuto zaidi na wanaoongoza kwa kupendwa na mashabiki.

1.DIamond platinum
Anaweza akawa sio muimbaji mzuri kama Alikiba au barnaba, ila haina ubishi huyu ndiye msanii wa kiume kwa upande wa bongo fleva anayeongoza kwa kupendwa zaidi na mashabiki, jina lake linazidi kukua siku hadi siku na kazi zake zinafanya vizur karibia east Africa nzima.

2. Wema sepetu
Sio muigizaji mzuri kumshinda Johari, wala hana filamu nyingi sokoni kuliko Irene uwoya, ndio maana hata waandaji wa tunzo za filamu hawajawahi kum nominate hata kwenye category ya msanii chipukizi bora, hiyo haijafanya jina lake lishuke kwenye Tasnia hiyo, Bado haina ubishi wema ana nyota Kali na anapendwa kuliko msanii yeyote. mwenyewe anajiita ENDLESS FAME.

3. LADY JAYDEE
Kiuno chake kina mfupa, hana mauno makali kumzidi Snura mushi, sauti yake nzuri na kipaji cha pekee alichobarikiwa kimemfanya apendwe zaidi na mashabiki kibao. Unadhani ana pesa sana kuliko ruge? Hakustahili kabisa kushindana naye , ila jeuri ya mashabiki aliyonao ilimfanya ajione malkia , nadhan unakumbuka Team anaconda ilifanya nini pale Nyumbani Lounge. Jide ana nyota Kali sana.

4. JB
Kipaji chake hakikumfikia marehemu kanumba(r.I.p),sio director mzuri kama Jackson kibirigi, ubunifu alionao kwenye filamu zake umemfanya apendwe zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa kiume kwa upande wa filamu apa bongo.

5.Lulu Michael
Hajawahi kuigiza vizuri kama Diana kimaro(Danija,Kigodoro) ila ana nyota nzuri sana, licha ya umri mdogo alionao , anapendwa na ana mashabiki wengi zaidi.

6.Monalisa
Hana umbo kama masogange, kipaji cha kipekee alichonacho na umakini alionao kwenye uigizaji umemfanya ajiongezee mashabiki wengi zaidi.

7. Ray kigosi
Sio muigizaji mzuri kumshinda Gabo, kampuni makini aliyonayo na aina ya waigizaji anaowatumia imemfanya kazi zake zinunuliwe zaidi kuliko kampuni yeyote apa bongo. Steps ilishawahi kusema kuhusu kazi za waigizaji zinazonunuliwa kama njugu, ray alishika namba mbili akitanguliwa na kanumba.

8.Johari
Hana swagger kama wema sepetu, kazi zake na umakini alionao kwenye uigizaji , vimemfanya apendwe zaidi na mashabiki , ndo maana hadi Leo kazi zake zipo juu.

UMEFANYa makosa kumsahau KING MAJUTO
 
Back
Top Bottom