Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
nilikuwa morogoro siku moja hivi, nimepanga lodge ya kawaida tu, nikasikia makelele reception kutoka nione nini, nikakuta Chid Benz, aisee, ni teja kabisa hadi anavoongea, ila cha ajabu, yupo na mwanamke wamekaa naye hapo karibia wiki, ila inavyoonyesha wote yeye na mwanamke ni mateja, ila mwanamke anatoka mambo safi na ni kama anamlea. anatia huruma mno. ni mgomvi dakika moja, sasa nilikuta anamgombeza dada wa reception na dada hajibu chochote, anadai amelipa pesa siku mbili kumbe hajalipa wala nini, na mwanamke anayeonekana alimpa hela alipe reception au sijui nini amesimama mlangoni na taulo tu anashangaa ugomvi. madawa ni kitu hatari mno.