Masuala haya ambayo MBOWE atayazungumzia kwenye mkutano na waandishi wa habari ni hadaa kwa umma.

Joined
Nov 27, 2019
Posts
35
Reaction score
146
Mkutano wa mwenyekiti wa Chadema FREEMAN MBOWE na waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika leo Februari 03, 2020 majira ya 5 asubuhi umejaa hadaa na upotoshaji kwa umma, nitafafanua kila jambo kwa hoja.

  1. Tume huru ya Uchaguzi.
  2. kamati ya Maridhiano
  3. Marekebisho ya katiba
  4. kuzuiwa kusafiri nje ya Nchi bila kibali cha mahakama
  5. kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mtaa
Kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali za mtaa, MBOWE anataka uchaguzi huo ufutwe wakati ulifanyika kwa mujibu wa sheria na yeye ndie aliyeagiza wagombea wa chama chake kujiondoa hali iliyosababisha wagombea wa CCM kupita katika baadhi ya maeneo kupita bila kupingwa. Hapa kama anataka kuupinga namshauri aende mahakamani.

Kamati ya Maridhiano, MBOWE anapaswa kufahamu siku zote serikali imekuwa ikiwapa nafasi wananchi wote kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi za vyama vya upinzani, dini, kabila n.k mara kadhaa tumemsikia Mhe. Rais akieleza yeye ni Rais wa wote. Tatizo lililopo ni kwa vyama vya upinzani kususisia kushirikiana na Serikali maridhiano ya KWELI yanapaswa kufanywa kwa vyama UPINZANI kuanza kushirikana na Serikali.

Tume huru ya uchaguzi, Tume inaweza kuwa na upungufu kama zilivyo za mataifa mengine, cha muhimu tukumbuke tume tulionayo ndio imeendesha uchaguzi wa 2015 na kupatikana kwa wabunge wengi wa upinzani tulionao Nchini akiwemo yeye, la muhimu Tume haiwezi kuisadia Chadema kushika dola bali Sera nzuri, Wanachama wengi na uzalendo kwa taifa.

Kuzuiliwa kusafiri Nje ya Nchi bila ya Kibali cha Mahakama, Mbowe anataka kutafuta huruma kwa masula ya kisheria, yeye na wenzake ni watuhumiwa, Mahakama imewapa dhamana kwa Masharti hivyo wanapaswa kuzingatia masharti hayo. Muhimu wajiepushe na ukiukwaji wa katiba na Sheria za nchi .

Marekebisho ya Katiba mataifa mbalimbali yamekuwa yakihusisha chanzo cha changamoto zinazowakabili na katiba, uhalisia ni kwamba Katiba PEKEE haiwezi kuwa mwarobaini wa matatizo yetu ya ukosefu wa huduma za kijamii kama elimu, afya na barabara n.k BALI viongozi imara, wazalendo, waadilifu, wachapa kazi kama Mhe. Rais Magufuli ndio watakaoleta maendeleo endelevu.
 
Tume huru ya uchaguzi wakati wabunge wengi wa upinzani wamepatikana 2015 kuliko kipindi chochote, mpaka wakajisifia kuwa Lowassa kawaongezea viti na kura za urais tofauti na walivyowahi kupata miaka yote.

Tunaoelewa mambo tunajua hizi ni mbwembwe za kuendelea kuwashikia akili wafuasi wao ili wabaki kuwa relevant.
 
Kitendo cha nchi kama "SWEDEN" kukata msaada kwa tanzania kwa 75% ndani ya miaka 5 ijayo (inaashiria wanapinga serikali ya jiwe), kwa mwenye akili ataelewa.

Kwanini miaka 5 ijayo???

Wanaangalia upepo kama sisi watanzania kama tutamchagua tena jiwe awe rais mwaka huu kwa mhula mwingine wa miaka 5 (au kama atatumia nguvu kuingia ikulu), kama atachaguliwa kua rais tena (kwa uchaguzi huru au nguvu) basi baada ya miaka mitano ijayo hawezi tena kugombea tena kikatiba (ndio warudishe misaada).

Na kama atatumia nguvu kurudi ikulu, basi hawa jamaa watatangaza vita au vikwazo "VIKALI ZAIDI" kwetu (pengine kama walivokutana navyo Zimbabwe).

Yajayo yanafurahisha.
 
Huyu mzee anatafuta kiki balaa, ameona zitto anapata wafadhiki na yeye anaamua kuokoteza propaganda ili na yeye walau asikike 😂😂 Siasa ngumu sana
 
Tume huru ya uchaguzi wakati wabunge wengi wa upinzani wamepatikana 2015 kuliko kipindi chochote, mpaka wakajisifia kuwa Lowassa kawaongezea viti na kura za urais tofauti na walivyowahi kupata miaka yote.

Tunaoelewa mambo tunajua hizi ni mbwembwe za kuendelea kuwashikia akili wafuasi wao ili wabaki kuwa relevant.
2015 rais hakuwa huyu ambaye anasema ole wake mkurugenzi amtangaze mpinzani ameshinda wakati analipwa mshahara na serikali ya ccm!
 
Wimbo wa Tume Huru ya Uchaguzi ulianza kabla ya 2015
 
Naona mnaelekea Kibra taratiiiiibu, haya ni Mateke ya Mwisho Mwisho ya Punda anayeaga Dunia.
Mtafurahi yani
 
Wimbo wa Tume Huru ya Uchaguzi ulianza kabla ya 2015
Uhitaji wa tume huru uneongezeka zaidi awamu hii ambayo Rais anatamani kuwe na chama kimoja na vingine vife!Ni wazi yuko tayari kuona anatumia nguvu ya vyombo alivyonavyo kuhakikisha wapinzani hawapati fair ground kwenye chaguzi!Tumeona kwenye chaguzi ndogo na uchaguzi wa serikali za mitaa!
 
mwana wa Tanzania,
Tatizo tunadhania kwamba kila anayekuwa m/kiti wa chama chochote, anakuwa na busara. Yaani nchi isubilie mtu wa uelewa ule na historia ile ya maisha akihutubia taifa! Sababu ni ipi? Mkiti wa chama? NO! Kuna viwango vya ufahamu vinavyotakiwa ili kuhutubia taifa.
 
Mkutano wa mwenyekiti wa Chadema FREEMAN MBOWE na waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika leo Februari 03, 2020 majira ya 5 asubuhi umejaa hadaa na upotoshaji kwa umma, nitafafanua kila jambo kwa hoja.

  1. Tume huru ya Uchaguzi.
  2. kamati ya Maridhiano
  3. Marekebisho ya katiba
  4. kuzuiwa kusafiri nje ya Nchi bila kibali cha mahakama
  5. kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mtaa
Kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali za mtaa, MBOWE anataka uchaguzi huo ufutwe wakati ulifanyika kwa mujibu wa sheria na yeye ndie aliyeagiza wagombea wa chama chake kujiondoa hali iliyosababisha wagombea wa CCM kupita katika baadhi ya maeneo kupita bila kupingwa. Hapa kama anataka kuupinga namshauri aende mahakamani.

Kamati ya Maridhiano, MBOWE anapaswa kufahamu siku zote serikali imekuwa ikiwapa nafasi wananchi wote kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi za vyama vya upinzani, dini, kabila n.k mara kadhaa tumemsikia Mhe. Rais akieleza yeye ni Rais wa wote. Tatizo lililopo ni kwa vyama vya upinzani kususisia kushirikiana na Serikali maridhiano ya KWELI yanapaswa kufanywa kwa vyama UPINZANI kuanza kushirikana na Serikali.

Tume huru ya uchaguzi, Tume inaweza kuwa na upungufu kama zilivyo za mataifa mengine, cha muhimu tukumbuke tume tulionayo ndio imeendesha uchaguzi wa 2015 na kupatikana kwa wabunge wengi wa upinzani tulionao Nchini akiwemo yeye, la muhimu Tume haiwezi kuisadia Chadema kushika dola bali Sera nzuri, Wanachama wengi na uzalendo kwa taifa.

Kuzuiliwa kusafiri Nje ya Nchi bila ya Kibali cha Mahakama, Mbowe anataka kutafuta huruma kwa masula ya kisheria, yeye na wenzake ni watuhumiwa, Mahakama imewapa dhamana kwa Masharti hivyo wanapaswa kuzingatia masharti hayo. Muhimu wajiepushe na ukiukwaji wa katiba na Sheria za nchi .

Marekebisho ya Katiba mataifa mbalimbali yamekuwa yakihusisha chanzo cha changamoto zinazowakabili na katiba, uhalisia ni kwamba Katiba PEKEE haiwezi kuwa mwarobaini wa matatizo yetu ya ukosefu wa huduma za kijamii kama elimu, afya na barabara n.k BALI viongozi imara, wazalendo, waadilifu, wachapa kazi kama Mhe. Rais Magufuli ndio watakaoleta maendeleo endelevu.
Pole ungejaaliwa hekima na busara, usingejiepusha kupiga ramli.
 
Hayo mambo unayoyaona ni hadaa kwa umma yanaweza kuwa unayaona hivo wewe tu au watu wa aina yako. Kuna watu wengine na aina nyingine wanaweza tu kuona kuwa ya na maana tofauti kwao.

Ninadhani ungejikita katika kuamua kumsikiliza au kutomshikiliza. Pia ukaheshimu haki ya wengine kumsikiliza au kutomsikiliza. Ukatambua pia haki ya Mbowe kuzungumza au kutozungumza. Tutambue na kuheshimu haki za wengine, kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom