Story kutoka mtandaoni Facebook 👇👇 Masudi anaelezea
"Siku moja mida ya usiku nipo maskani tumepaki bodaboda zetu na washkaji zangu ikaja gari ikapaki pembeni ya bodaboda zetu. Ndani kulikuwa na jamaa.
Sisi tuliendelea na story zetu. Ghafla akaja binti mmoja wa pale kitaani kwetu akaingia kwenye ile gari. Binti mwenyewe anatufanyia mashauzi sana dereva bodaboda wa pale maskani.
Baada ya kumaliza kuongea kwenye gari lao binti akashuka ikabidi jamaa aondoke, sasa kwa bahati mbaya wakati anarudi nyuma ili apate kutoka vizuri pale parking akasukuma pikipiki yangu.
Pikipiki haikuumia sana, ilipata michubuko kidogo tu. Kuona vile wadau wangu si wakakiwasha kwa jamaa. Kwanza amekuja kitaani kwetu kututambia halafu na demu wake mwenyewe anajikuta mashauzi, basi ni kama tulikuwa tunamaliza hasira za yule kwa mshkaji.
Kutokana na sapoti ya wadau wangu na mimi nikajaa upepo, tukamwambia hatoi gari mpaka alipe laki na nusu. Hapo mimi na wanangu hatutaki kuelewa tunataka hela tu.
Jamaa alikuwa mstarabu sana aisee. Alituomba sana kuwa hana hela kwa muda ule kwahiyo atuachie elfu hamsini na ukizingatia pikipiki haijahariba sana. Bado tukakaza, kwa fujo tulizomfanyia nahisi kweli hakuwa na hela ikabidi mwisho wa siku tumchukulie hiyo elfu hamsini yake.
Si unajua mkiwa kampani ni mikwala mingi na meneno ya kujimwambafai ili tumchukulie points mbele ya demu wake. Jamaa kinyonge akaondoka baada ya kutuachia ile hela. Tukajiona tumeshinda.
Sasa kesho yake nikapata mteja wa kumpeleka Milambo kwenye ile kambi ya jeshi. Yule dada ni mpishi mule ndani kwahiyo hata sikuwa na wasiwasi nipo na mwenyeji.
Sasa kufika getini tukasimama, yule dada akawa anasalimiana na wanajeshi wa pale mlangoni. Kwa mbali kulikuwa na askari ananiangalia sana ila hata sikumzingatia. Tukapita vizuri bila shida.
Baada ya kumfikisha ilibidi nirudi mwenyewe, kufika pale getini yule afande aliyekuwa ananiangalia sana akanisimamisha. Alikuwa mbali kidogo ilibidi anifuate.
Baada ya kufika akanisalimia, ile kuitikia tu akasema "Ah kumbe ni mwenyewe" nikawa nashangaa mwenyewe mwenye nini?. Akasema alidhani ananifananisha ila sauti yangu imeniponza.
Akaniuliza unanikumbuka?. Alvyomaliza swali tu fahamu ndio zikanijia kumbe ndio jamaa niloyesumbuana nae jana usiku. Aloo jasho likaanza kutoka ghafla ikabidi nikatae kuwa simjui.
Akaniambia anaomba leseni, sikuwa nayo. Akaniomba kitambulisho chochote, sikuwa navyo pia. Akaniambia leo umejichanganya shuka kwenye pikipiki nifuate.
Ikabidi nipaki boda halafu taratibu namfuata kwa nyuma. Akageuka akaniambia kwa unanifuata nyuma kama mkeo? ebu chuchumaa halafu jichagulie mwenyewe mwondoko wa kunifuata hivyo hivyo. Dahh! Ikabidi nijiongeze niruke kichura chura huku nikimfuata.
Akanipeleka kwenye nyasi ndefuu.. akaniambia jana nishakulipa hela leo ndio utaifanyia kazi. Sasa inabidi ufyeke hili eneo lote.
Akaniambia kama naweza niwapigie washkaji zangu waje wanisaidie na kufyeka ni ruksa.
Dahh palikuwa palefu aisee. Ningefanya nini? kinyonge nikaanza kufyeka.Baadaye akaja afande mwingine, alionekana mstaarabu sana nikasema hapa ndio pakujiliza ila aniombee msamaha. So ikabidi nimwambie jamaa amenionea amenipa eneo kubwa kisa tu sijaingia na kitambulisho mule ndani.
Akaniuliza.. amekuonea?. Nikajibu ndio. Akasema basi mimi sitakuonea nitakupa kipande unachostahili ili usirudie tena. Akaniongezea kipande kikubwa zaidi.
Niliingia mida ya saa nne. Nilifyeka mpaka saa 11 inaenda saa 12. Nimetoka hapo nikaenda kuoga na kulala kabisa". Masoud, Tabora.
WatuNiStory