Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,968
- 8,139
Kesi kama hizi ndo CMA wanazipenda sana.Operations Manager alitumia msahafu kuwafukuza kazi vijana waliyeleta mteja kwenye kampuni yake bila kuangalia aina ya kosa na athari zake kwa kampuni; hakujali wala kuangalia uzoefu wa wakosaji wahusika, hakujali historia yao ya kufanya makosa, umuhimu wao kwenye biashara, athari zinazoweza kutokana na kufukuzwa kwao kazi kwa kampuni na kwa wateja na mambo mengine
Wapo managers wengi sana wa aina hii. FUSO endelea na haka kahadithi tujue iliishaje
Na ma managers wa aina hii ni tatizo kubwa sana kwenye organisations nyingi. Wengi ni wala rushwa na wahujumu, sasa kuwafukuza vijana kazi inawezekana ilikua matokeo ya hasira ya kukosa 10%Kesi kama hizi ndo CMA wanazipenda sana.
Acha kujidai mjuaji wa kila kituHahaha kwa hiyo CEO akasema "Laura take care of THIS young boys" au siyo?
Na nyinyi mlikua wawili? Halafu ni "... THIS young boys"
Binti acha kudandia wanaumeAcha kujidai mjuaji wa kila kitu
Nikasikia kwa mbali OP akisema you need to see the company secretary immediate after this...wakatoka wakatuacha - tulibakia pale conference kwa muda kama nusu saa, nikazinduka nikamshtua mwenzangu nikamwambia kaka jikaze huu ndiyo ukubwa, tayari tushaingia cha kike - wamesema tukamwone secretary pale chini hatuna namna... Kosa letu kubwa tunatuhumiwa nalo kujaribu kujipatia commission bila kufuata utaratibu... tume pindisha deal kwa makusudi ili tujipatie fedha huku tukijua kufanya hivyo ni kosa kubwa.
Tulitoka huko, baadhi ya staff wakitushangaa mno kulikoni?? maana hatuwashirikisha kwa lolote kwa hiyo hawakujua what is going on...
Tulifika pale reception, tukakuta barua tayari zilishachapwa na kusainiwa tayari kwamba kwa kosa tulilofanya hatuwezi kuvumilika hivyo sisi si wafanyakazi tena wa kampuni kuanzia muda huo - tutapewa mshahara wa mwezi mmoja kama sheria inavyotaka na tunatakiwa kukabidhi vitu vya office siku hiyo hiyo na kuondoka.
Aisee nilitamani nife kabisa, niliona maisha yangu hayana maana tena - nilifikiria je ntalipaje pango, nitakula nini? maisha magumu.. kikakabidhi vitu vyao nikachukua barua yangu ya kufukuzwa nikasepa - mshikaji wangu pia hivyo hivyo tukaondoka - kabla ya kuagana kituo cha basi tukapanga tukutane kesho getoni kwangu tupange nini cha kufanya......
....inaendeea usiondoke