...tunaendelea tulipoishia...
Jamaa yangu alifika asubuhi saa tatu, tulianza mjadala moja kwa moja - mjadala ulikuwa mgumu na fikirishi mno - Hoja mezani zilikuwa Je twenda kuomba msamaha au lah? Je kuna uhumimu gani au faida gani tutapata endapo tutaomba msamaha? Je ni hasara ama faida endpo hatutakwenda kuomba msamaha ? Je msamaha wenyewe ni wa kurejeshwa kazini ama ni wa kutusafisihia tu CV zetu zilizochafuka? Je ni nani tunakwenda kumwomba msamaha huo, ni CEO ama ni line manager wetu?
Tulivutana mno, mwenzangu alishauri tuachane nao na maisha yaendelee kwamba hakuna haja ya kumpigia magoti mwanadamu, sisi bado vijana na tuna future kubwa mbele yatu ukizingatia kozi tulizo soma zina uhitaji (market) kubwa. Mimi nani nilisimamia msimamo kwamba ni sawa anavyopendekeza ila umuhimu wa kusafisha majina yetu ni mkubwa mno kwa maana kokote tukakapokwenda tutaulizwa previous job reference, tumefanya kazi wapi na wale watu wanaotaka kutuajiri watahitaji kupata fununu juu ya tabia zetu na utendaji wetu wa kazi.
Mjadala ulikwenda hadi alasiri, tunasikia njaa tukaamua tutoke kwende pale Rose Garden, si mbali sababu wote tulikuwa tunaishi Sinza na kwa wakati huo kiwanja hicho kilikuwa ndiyo makutano ya hasa vijana kubadilishana mawazo huku walipata chakula... Tulikaa wenyewe tu ili tumalizie mjadala wetu na kabla ya siku kuisha tuwe na msimamo mmoja.
Baada ya chakula tuliendelea na mjadala huku tukigonga glass moja moja tukipeana matuamani ambayo ki ukweli hayakuwepo, mwishoni tukaafikiana twende tukaombe msamaha kwa CEO kesho yake na si kwa line Manager wetu sababu kuu kwamba yeye ndiye aliyelishughulikia jambo letu toka mwanzo - na msamaha tunaokwenda kuomba si wa kurudishwa kazini hapana ila tu ni wa kusafisha CV zetu ili tupate reference nzuri endapo zitahitajika na waajiri wengine. Hoja ya mwisho ilikuwa tunakwenda kwa CEO ofisini kwake ama nyumbani kwake? hapa napo tulivunata mno, kwa kauli moja tukaafikiana twenda nyumbani kwake badala ya ofisini - twende kama vijana wake..tuliona ni rahisi kumpigia magoti CEO kuliko line manager wetu. Tuliagana pale mida ya saa mbili usiku kila mmoja akienda getoni kwake kupumzika.
Inaendelea.......