Maswali fikirishi kuhusu Ubongo wa mwanadamu

Maswali fikirishi kuhusu Ubongo wa mwanadamu

Mbongo usichanganye mambo, alafu usije na speculations zako huku huna hata simple idea computer inaprocess vipi information, we unauhakika unaweza kuishinda computer calculations?

Kukosekana efficient algorithms ambazo zinadeal na computer vision kutambua kua object flani ni kitu fulani haimaanishi ubongo unafanya more calculations than human, it simply means we process information differently.

Usikae kuniambia kwa taarifa yangu ati the top notch machine inazidi nzi mara 10K, ninafahamu computer vizuri zaidi ya uijuavyo wewe, huu ubishi wa jf watu msio na idea mnachokiongea hua siupendi.

Nenda fanya calculations kwa kichwa kujua the exact position ya satellite, exact angle, exact speed at each milliseconds ikiwa inazunguka dunia uniambie kama utashindana na computer ambayk inakufanyia hiyo calculation in milliseconds, wewe hadi ushike kalamu na karatasi hadi unamaliza kucalculate moja computer ishakuletea results zaidi ya milioni..
Au uwekewe ramani ya jiji upewe stations 200 uambiwe tafuta njia fupi kutoka sehemu A00 kwenda sehemu Z00 uone itakavokuchukua siku nzima, computer itarudisha jibu kwa sekunde.

Na kama bado ni mbishi sana kwa kua wanaJF ndivyo mlivyo, nikupe hesabu alafu niandike computer algorithm ya kufanya hiyo hesabu alafu tukushindanishe wewe na computer tuone. Swali jepesi tu hata nisiende mbali, nakupa squares 500 zenye length na width tofauti, nataka unirudishie area ya kila square, formula ya area ni length x width, wewe zidisha kwa kila square hadi unafika square la 500 itakua giza lishaingia, computer itafanya yote haya na kunipa jibu chini ya sekunde moja.
kabla ya computer kufanya kazi yote hiyo binadamua alishika kalamu akafanya calculations akafikiesha akili yake matokea yake yakawa hayo unayo yasema "think twice"
 
Ntajibu maswali yako mengine yote kwa kua ni interesting na majibu yake ninayo.. Ila napenda nianze na hilo la tatu kwa sababu computers fascinate me than anything else.

Computer inaweza kutambua harufu, ila kabla hatujaenda inatambuaje harufu labda nikueleze kidogo computer imeundwaje kwa undani kidogo sana japo ntaacha mambo mengi kwa kua ni vitu vinaweza kukuchanganya viko very complex.

Kuna kitu kinaitwa "binary digits" hizi ni namba 0 na 1. Kila computer au logic device yoyote duniani, inatambua hizi namba mbili peke yake, picha zote unazoona kwenye monitor, maneno yote unayoandika kwenye keyboard, miziki, video, movies, messages e.t.c, vyote hivi kiundani ni information ambayo inatunzwa kama 0 au 1 peke yake.

Kama kwenye switch 0 inamaanisha off, na 1 inamaanisha On, kwenye 0 na 1 unaweza kurepresent namba nyingi, watu wa kawaida huhesabu 0,1,2....9 na kurudi 10, 11... kwenye computer tunahesabu 0, 1, 10, 11, 100, 101, 110, 111 sijui kama umeona pattern hapo, kama 4 ya decimal, kwenye binary ni 100, 5 - 101, 6 - 110...... Ndani ya computer kuna vidude vidogo sana vinaitwa transistors, kama kwenye processor yako vinaweza kua hata bilioni vimejazana, vyenyewe kazi yake hasa ni kuwa on (1) au kua off (0) basi, Hizi transistors ndio building blocks za computer na logic device zote dunia nzima. Sasa kujua calculations zinafanyika vipi huko ndani sitoonglea maana hadi hapa naweza kua nshaanza kukuchanganya ila ukiitaka kujua uniulize.

Sasa nikupe mfano hizi namba zinageukaje hadi unaweza kuona kitu kwenye computer, chukulia mfano wa monitor yako, kuna pixels nyingi ndogondogo, hizi ndizo zinazobadilika rangi hadi unaweza kuona maandishi au kitu chochote unachoona kwenye screen, kila pixel inatoa rangi flani, sasa computer yenyewe nilisema inatambua namba peke yake, hata rangi pia ziko represented in numbers, kumbuka rangi nyeupe inatokana na muunganiko wa red, green na blue, nyeusi maana yake hakuna rangi, rangi nyingine za katikati zinatokana na mchanganyiko wa hizi rangi tatu (RGB), computer inatunza rangi katika namba, RGB, mfano nyeupe ni 255-255-255, maana yake umechanganya red,green na blue katika range sawa (255), tukija 255-0-0, hiyo ni red, kwa kua red ina 255 ila green na blue ni 0, 255-255-0 hiyo ni yellow (red na green 255 ila blue 0).... Kwa hiyo computer yenyewe inatuma tu signal kwenye monitor, hiyo signal ichukulie kama namba, monitor inafanya calculations inatoa hiyo rangi inayotakiwa kama mfano niliokupa.

Sasa turudi kwenye harufu, Computer inapata data za nje kutokana na sensors mbalimbali, picha toka kwenye camera, sauti kwenye mic, joto kwenye digital thermometer e.t.c, ila vyote hivi vikiingia kwenye computer narudia data zake zinatunzwa kama 0 au 1, digital thermometer ikisoma joto degree 20, inaweza pitisha data kama 10100.
Harufu nayo data zake zinatunzwa hivohivo, kunakua na sensor, kama ya harufu wanaiita e-nose, yenyewe inaangalia chemical composition ya harufu, inasoma pattern yake alafu inatunza hiyo pattern katika binary.. Ukiiiweka kwenye harufu tofauti, itafanya process hiyohiyo, tuseme mfano harufu A inatunzwa kama 100001, harufu B inatunzwa kama 111100, hiyo sensor ukiipitisha tena kwenye harufu A, pattern itarudi ileile ya 100001, kwa kua tushaiambia computer kua ukiona 100001 hiyo ni harufu A, basi computer itakujibu kua ni harufu A ila in reality haina akili kua inajua harufu, inarudisha hilo jibu kwa kua tumeiambia tu kua ukiona 100001 we sema harufu A, haijui harufu ni nini.

Ukiwa unaiangalia computer, usifikirie ina akili kama binadamu, yenyewe ni switch tu ambazo ziko either on au off, kutokana na hizo switch sisi ndio tunafanya kitu kinaitwa "abstraction" tunacommand kua ukiona kitu flani fanya kitu flani, haiwezi kwenda tofauti na tulivyosema, haina akili ya kujiamulia.

Sasa hivi tulipofikia kwenye technology, bado computer ina shida kutambua kua huyu ni mtu, au hili ni gari, kumbuka kila kitu ndani ya computer ni namba 0 au 1, kuchukua picha ya mtu, zile rangi ukasema ubadilishe uweze kutambua kua huyu ni binadamu, hesabu za hapo sio za kitoto, ni research imeendelea kwa miaka zaidi ya 40, ingawa inajitahidi kidogo siku hizi ila still haiko accurate. Kwa mambo mengine computer inaweza kazi vizuri mno kuliko hata binadamu, ukiambia kitu yenyewe itafanya exactly kama ulivyoiambia.

Pole kwa maandishi marefu, nimetafuta lugha rahisi zaidi kuelezea hili nimeshindwa, ingekua mtu wa computer ningeweza kumuelezea kwa ngeli na kiundani zaidi. Ila i hope umetoka na kitu angalau cha juu juu.
kama ni mtihani kwa hayo maelezo nakupa 15%
 
Back
Top Bottom