Maswali kwa mkurugenzi wa HESLB ndugu Badru

Especially continues walio pata kwenye batch ya mwisho hamna alie pewa pesa zake.sasa nashangaa kutoka mwezi wa 11 hadi leo Office kama iyo ina shindwa vipi kuwahisha mambo ..hili ni jipu kweli

Hivi hamna mfanyakazi wa bodi humu ajibu
Wataongea uharo hata wakipewa hiyo chance,wakaetu kimya na roho zao mbaya wakisubiri utenguzi
 
sometimes hua ni tatizo la chuo na sio board, nakumbuka nilikua nasoma DMI wale wahindi walikua wanaweka hela kwenye fixed account. Mnasaini then mtasubiri, mtalia hadi machozi yakauke ndio mnawekewa fedha zenu
 

Yani tatizo Ni kubwa kwa vyuo vyote. Hapa UDSM Hali sio nzuri. Kama pesa hakuna wangesema. Bodi imeonesha udhaifu mkubwa Sana.
 
sometimes hua ni tatizo la chuo na sio board, nakumbuka nilikua nasoma DMI wale wahindi walikua wanaweka hela kwenye fixed account. Mnasaini then mtasubiri, mtalia hadi machozi yakauke ndio mnawekewa fedha zenu
Hilo pia linawezekana ila kama zimewekwa fixed account itakua ni hao bodi.
 
Yani tatizo Ni kubwa kwa vyuo vyote. Hapa UDSM Hali sio nzuri. Kama pesa hakuna wangesema. Bodi imeonesha udhaifu mkubwa Sana.
Halafu wanajisifu eti wameongeza idadi ya wanufaika.
Ninawashangaa watu wasanii hawa mbele ya kamera
 
sometimes hua ni tatizo la chuo na sio board, nakumbuka nilikua nasoma DMI wale wahindi walikua wanaweka hela kwenye fixed account. Mnasaini then mtasubiri, mtalia hadi machozi yakauke ndio mnawekewa fedha zenu

Kwa Sasa pesa haijawekwa mkuu. Ni vyuo vyote vya umma na binafsi.
 
Mara nyingi kucheleweshwa kwa hizo fedha inasababishwa na chuo. Unakuta mtu kwenye form aliandika anasoma miaka mitatu, akifika chuo anabadili anaenda kozi ya miaka minne. Mwaka wa tatu wanakoma kumpa hela. Mpaka waje kuhakikisha bado ni mwanafunzi sio jambo la haraka.

Vyuo vingine kama NIT ukipata supp unachelewa sana kupata mkopo. Wao wanafanya sup baada ya field kuisha, matokeo mpaka yaje kufika bodi vyuo vilishafunguliwa.

Vyuo vingine wazembe tu. Mbona Tumaini ya DSM huwa wanawahi kupata. Yani vyuo vingine wanafunzi wanasubiri zaidi ya siku 10 ila Tumaini wako kasi kwenye hela za watu.

Alafu sio kazi rahisi kutoa hizo hela mara zote kwa wakati. Tukubali tu sometimes kuna changamoto kidogo
 
SERIKALI IMTAFUTE WA KUWAJIBIKA. AU WOTE WANAFANYIA FEDHA ZA WANUFAIKA BIASHARA.
UZEMBE UNASABABISHWA NA NINI?
 

Mkuu ulichosema Ni kweli, lakini kwa tukio la Sasa pesa haijawekwa vyuo vyote. Watu wamesin Ni wiki ya pili Sasa lakini pesa hamna.
 
Rest Easy hero JPM

Hili neno dogo liandikwapo linabeba maumivu ya dhati ya mwandishi.

Hii nchi vilio vya kipuuzi hivi vilikoma hadi watu wakaanza kuhoji mbona kila kitu kiko sawa hiviii, hela zunatoka wapi,?

Shida sio hela shida ni mtu anaeongoza hela
 
Je kwanini bodi haiwapi wanachuo hela za mwaka wa kwanza ambao wapo mwaka wa pili.
Hii inatokea kwawale waliokata rufaa wakapangiwa lakini hawajapewa. Nini tatizo
 
Mkuu pole ila umeandika kwa hisia sana bila kuzingatia kuwa yawezekana shida ipo chuoni kwenu.

1. Amini kuna vyuo vinachukua fedha alafu vinafanya kuizungusha kwanza alafu lawama zinaangukia HESLB

2. Amini kuna vyuo vinachelewesha sana kuwasilisha majina yaliyosainiwa HESLB hivyo fedha nayo haitoki

3. Amini kuna vyuo vinachelewesha kutuma taarifa za matokeo ya wanufaika hasa wanaoendelea na masomo nayo inachangia fedha kuto kutoka kwa wakati.

Sidhani kama chuo kikikamilisha mambo yote yanayotakiwa kuwasilishwa HESLB fedha itachelewa kutoka tena kwa chuo kimoja au viwili ni ngumu sana labda kwa vyuo vyote na hapo ni labda fedha hamna.

Angalia pande zote Mkuu, ni vizuri uzi wako ungeuandika kama kuhoji na ungetaja chuo na mazingira sio lawama kwa wahusika alafu ukute wala hawahusiki na huu uzembe, watakuona mjinga.

Ila Mkuu pole sana!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…