Mkuu pole ila umeandika kwa hisia sana bila kuzingatia kuwa yawezekana shida ipo chuoni kwenu.
1. Amini kuna vyuo vinachukua fedha alafu vinafanya kuizungusha kwanza alafu lawama zinaangukia HESLB
2. Amini kuna vyuo vinachelewesha sana kuwasilisha majina yaliyosainiwa HESLB hivyo fedha nayo haitoki
3. Amini kuna vyuo vinachelewesha kutuma taarifa za matokeo ya wanufaika hasa wanaoendelea na masomo nayo inachangia fedha kuto kutoka kwa wakati.
Sidhani kama chuo kikikamilisha mambo yote yanayotakiwa kuwasilishwa HESLB fedha itachelewa kutoka tena kwa chuo kimoja au viwili ni ngumu sana labda kwa vyuo vyote na hapo ni labda fedha hamna.
Angalia pande zote Mkuu, ni vizuri uzi wako ungeuandika kama kuhoji na ungetaja chuo na mazingira sio lawama kwa wahusika alafu ukute wala hawahusiki na huu uzembe, watakuona mjinga.
Ila Mkuu pole sana!.